• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Biteko aitaka CWT kuendana na kasi ya mabadiliko duniani

Posted on: October 16th, 2025

BITEKO AITAKA CWT KUENDANA NA KASI YA MABADILIKO DUNIANI 

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Dotto Mashaka Bitteko leo tarehe amefungua semina ya viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Kanda ya Ziwa na Kanda ya Ziwa Magharibi na kukitaka CWT kubadilika kulingana na kasi mabadiliko yanayoendelea kutokea duniani.

Akizungumza katika hafla ya ufunguzi ilichofanyika katika ukumbi wa Mwembeni Complex, Mhe. Biteko amesema dunia ya leo ina kasi kubwa mnatakiwa kuwafikia walimu wakati wote wawasikilize na muwape sababu ya walimu kuwapenda ninyi na kwa kuwahudumia watarudi kwenu.

“Tumetoka mbali,------mbinu zilizotumika miaka mitano, kumi iliyopita haziwezi kuendelea kutumika katika dunia ya leo” amesema Mhe. Biteko na kuongeza kuwa “endeleeni kuishi kwa dunia inayobadilika, fikilini upya kila siku”.   

Mhe. Biteko amesema mabadiliko ya dunia yanawasukuma watu kufikiri sana tena kwa haraka na viongozi wa CWT wanapaswa kujua walimu wanaowaongoza kwa sasa sio kama walimu wa zamani kwa sababu walimu wa sasa ni watu wanaohoji sana, na sio kwamba hawaridhiki ni kwa sababu dunia iliyopo ni dunia inayobadilika.

“Mnapaswa kutambua kuwa kwa kubadilika kwa dunia na ninyi staili yenu ya uongozi lazima ibadilike ili kuweza kuwahudumia walimu vizuri” amesema mhe. Biteko.

Mhe. Biteko ametoa mifano ya mambo mbalimbali yaliyobadilika duniani ambayo wakati huo yalionekana muhimu sana, lakini kwa sasa hayahitajiki tena na kuitaka CWT kubadilisha staili yao ya uongozi ibadilike kuendana na mabadiliko ya dunia.  

Mhe. Biteko ametumia fursa hiyo kukishukuru CWT kwa mafunzo ya uongozi na fursa mbalimbali alizowahi kuzipata akiwa kiongozi wa chama hicho katika Mkoa wa Geita kabla ya kuingia katika siasa.

Aidha, Mhe. Biteko amekihakikishia CWT kuwa Serikali ya awamu ya sita inathamini kazi kubwa inayofanywa na walimu katika maendeleo ya nchi ya Tanzania na inatatua changamoto za walimu kulingana na hali ya uchumi inavyoruhusu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Patrobas Paschal Katambi, amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeboresha masuala mengi yanayotatua changamoto za walimu hapa nchini.

Mhe. Katambi ameyataja masuala hayo kuwa ni pamoja na kufanyia marekebisho sheria mbalimbali, uboreshaji wa miundombinu ya shule, upandishwaji wa madaraja, mishahara na kulipa madeni ya watumishi ikiwemo walimu.

Mhe. Katambi amewataka walimu kuendelea kutoa huduma kwa weledi na kushirikiana na Serikali ili kuweza kutatua changamoto walizonazo ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba za kuishi na kuwaboreshea mazingira ya kufanyia kazi.  

Kwa upande wake, Katibu wa CWT Mkoa wa Mara ambaye pia ni Katibu wa CWT Kanda ya Ziwa na Ziwa Magharibi Ndugu Morgson Kabeho amesema semina hiyo imehusisha viongozi wa CWT kutoka mikoa nane ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Ziwa Magharibi yenye wilaya 51.

Ndugu Kabeho amesema jumla ya viongozi wa CWT 450 wameshiriki mafunzo hayo na kuongeza kuwa CWT inaamini baada ya mafunzo viongozi hayo viongozi hao watakuwa na uwezo mzuri zaidi wa kuwahudumia walimu.

Semina hiyo yenye kauli mbiu “Ni Jukumu letu Walimu kushiriki Uchaguzi Mkuu 29/10/2025 kwa Maendeleo, Amani na Utulivu wa Nchi yetu” imewahusisha viongozi wa CWT kutoka Mikoa ya Mara, Mwanza, Tabora, Kagera, Kigoma, Simiyu, Geita na Shinyanga

Ufunguzi wa semina hiyo umehudhuriwa pia na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Mhe. Patrobas Paschal Katambi, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya, viongozi wa CWT Taifa na Kanda ya Ziwa na Ziwa Magharibi, viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Demokrasia inaendelea kupevuka katika Mkoa wa Mara: Mtambi

    October 16, 2025
  • Biteko aitaka CWT kuendana na kasi ya mabadiliko duniani

    October 16, 2025
  • RC awapokea Maafisa na wanafunzi kutoka Chuo cha Jeshi cha CSC

    October 13, 2025
  • RC awapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 Mara

    October 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa