Benki ya Dunia imeridhishwa na utekelezaji wa afua nane za Mradi wa BOOST unaolenga kuboresha elimu ya awali na msingi katika Mkoa wa Mara.
Akizungumza katika kikao cha majumuisho ya ziara ya ufuatiliaji iliyofanyika katika Mkoa wa Mara, Mtaalamu wa Benki ya Dunia Bibi Gemma Todd ameupongeza Mkoa wa Mara kwa usimamizi na kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi kwa kiwango na kwa wakati.
Aidha, Bibi Todd amepongeza kwa namna Mkoa unavyotekeleza mradi huo kwa ufanisi na kwa ushirikiano kutoka kwa maafisa wa taaluma mbalimbali jambo ambalo limefanikisha utekelezaji wa mradi huo kwa kiasi kikubwa.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na maafisa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais TAMISEMI, maafisa wanaosimamia mradi huo ngazi ya Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa