Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Adam Kighoma Ali Malima ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuandaa mpango wa kulipa madeni na kuuwasilisha katika ofisi yake ndani ya siku 14.
Agizo hilo amelitoa leo tarehe 9 Juni 2020 wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Tarime kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali kwa mwaka 2018/2019.
“Mpango wa kulipa madeni uwasilishwe ofisini kwangu ndani ya siku 14 ili yalipwe kwa haraka kabla halmashauri hiyo kuwa na madeni mengi yasiyolipika” alisema Malima.
Aidha amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kutenga fedha na kuweka vifaa vya zimamoto kwenye sehemu muhimu kama vile stoo na ofisi haraka iwezekanavyo.
“Haiwezekani halmashauri isiwe na vifaa vya zimamoto sehemu zote hata sehemu muhimu, sasa angalieni cha kufanya vipatikane haraka” alisema Mheshimiwa Malima.
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2018/2019 ilipata hati safi na kuwa na hoja 41mpya na hoja za miaka ya nyuma 19.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa