Jumla ya wananfunzi 83,558 wanatarajiwa kufanya Mtihani wa Taifa wa Upimaji kwa Darasa la Nne kwa mwaka 2024 katika Mkoa wa Mara ulioanza leo tarehe 23 Oktoba, 2024 hadi tarehe 24 Oktoba, 2024.
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ina watahiniwa 14,465, Halmashauri ya Wilaya ya Rorya in watahiniwa 13,875, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti in watahiniwa 11,276 wakati Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ikiwa na watahiniwa 9,513.
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ina watahiniwa 9,162, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ina watahiniwa 7,988, Halmashauri ya Mji wa Bunda ina watahiniwa 6,642, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma ina watahiniwa 5,612 huku Halmashauri ya Mji wa Tarime ikiwa na watahiniwa 5,034.
Bwana Bulenga ameeleza kuwa mitihani hiyo inasimamiwa na Kamati za Uendeshaji za Mikoa/Halmashauri ambazo zimepewa mamlaka na Sheria ya Baraza la Mitihani Sura 107 ya mwaka 1973 na marekebisho yake ya mwaka 2019.
Bwana Makwasa amesema hadi sasa maandalizi kwa ajili ya ufanyaji wa mtihani huo yamekamilika ikiwemo pamoja na semina kwa wasimizi wa mitihani zimeshafanyika na vifaa vyote vya mitihani vimeshapokelewa katika Mkoa wa Mara na kusambazwa katika Halmashauri za Mkoa wa Mara.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa