Jumla ya wanafunzi 24, 138 kutoka Mkoa wa Mara wanatarajiwa kufanya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne kwa mwaka 2023 unaoanza leo tarehe 13 Novemba, 2023 hadi tarehe 30 Novemba, 2023.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu na Mafunzo Bwana Makwasa Bulenga imeeleza kuwa maandalizi yote kwa ajili ya kufanya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kupokea vifaa vya mitihani na kukabidhiwa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa wa Mara.
Taarifa hiyo inaonyesha kuwa Mkoa wa Mara una jumla ya shule na vituo vya kufanyia mtihani huo 242 ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ina shule 46, Halmashauri ya Wilaya ya Tarime 43, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti 38, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma 25 na Halmashauri ya Wilaya ya Butiama 21.
Nyingine ni Halmashauri ya Wilaya ya Bunda 20, Manispaa ya Musoma 19, Halmashauri ya Mji wa Bunda 16 na Halmashauri ya Mji wa Tarime yenye shule 14.
Taarifa hiyo imeonyesha kuwa jumla ya wasimamizi 724 wanatarajiwa kuhusika kusimamia mtihani huo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa