Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Mkoa unakadiriwa kuwa na jumla ya ng’ombe 1,651,355, mbuzi 757,428, kondoo 402,492 na kuku wapatao 1,612,672. Idadi kubwa ya mifugo hiyo inapatikana maeneo ya vijijini ni Ng’ombe 93%, mbuzi 95.6%, kondoo 97.5% na kuku 92.1% na mifugo mingine ikipatikana maeneo ya mijini. Mkoa wa Mara kuna livestock units 676,160 ambazo zinahitaji eneo la malisho Hekta 1,081,857. Eneo lililopo kwa ajili ya malisho ya mifugo ni hekta 750,000 hivyo kuna upungufu wa maeneo ya malisho hekta 405,697. Hii ina maana kwamba mifugo iliyopo katika Mkoa wa Mara ni mingi ukilinganisha na eneo la malisho lililopo.
Mkoa una hekta 43,170 ambazo zimetengwa na kupimwa kwa ajili ya malisho (Rorya ha 5,400, Bunda ha 743.2, Butiama ha 320, Musoma ha 150, Tarime ha 4,800 na Serengeti ha 31,757). Uendelezaji wa nyanda za malisho unafanyika zaidi kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa ambao hutumia ufugaji wa ndani, kwa ng’ombe wa nyama uboreshaji unaenda taratibu kutokana na uchungaji huria. Mikakati ya kukabiliana na hali hii ni Serikali za Vijiji kuainisha matumizi bora ya Ardhi kwa kila Kijiji, kuendelea kuvuna mifugo na kuiuza minadani, kuboresha Koo safu za Mifugo, kuendelea kuelimisha wafugaji juu ya ufugaji wa ndani (zero grazing) pamoja na kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji.
Kwa upande wa miundombinu ya mifugo Mkoa wa Mara una jumla ya Majosho 162 (64 mazima, 48 hayafanyi kazi, 43 yanahitaji ukarabati na 7 ni ya watu binafsi), Vibanio 82, Malambo 145 (135 mazima na 10 mabovu), Mabwawa 3, Minada 29, Vituo vya Afya ya Mifugo 33, Machinjio 28, Mashamba ya Mifugo 6, Vituo vya Kukusanyia Maziwa 22 na Matanki ya Kupozea Maziwa 3, Mabanda ya Ngozi 18, Holding Ground 1 na Mnada wa Upili 1. Uwepo wa miundombinu hii imesaidia katika kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo na hivyo kuboresha lishe na vipato vya wafugaji.
CHANGAMOTO
Pamoja na ustawi wa sekta ya Mifugo Mkoani bado kuna changamoto kadhaa zinazoathiri ukuaji na tija ya sekta hii ziwemo:-
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mkoa umeweka mikakati ifuatayo:-
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa