• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi afanya ziara Butiama

Posted on: January 20th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Evans Alfred Mtambi leo tarehe 19 Januari, 2025 amefanya ziara katika Wilaya ya Butiama ambapo ametembelea Mgodi wa Bernard Kitamala uliopata usaidizi wa kiufundi kutoka Kampuni ya Shoucheng (T) Co. Ltd kutoka China.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa ya mgodi huo, Mhe. Mtambi ameuongeza mgodi huo kwa kupanga kuanzisha Kiwanda cha kuchenjua Dhahabu ambacho kitatumika pia na wachimbaji wadogo wa madini waliopo katika eneo hilo kuchenjua dhahabu zao.

“Ninawapongeza sana kwa kuanzisha kiwanda cha kuchenjua dhahabu, najua hii itawasaidia wachimbaji wadogo wa eneo hili kupata sehemu ya jirani ya kuchenjua dhahabu zao” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka Watanzania waliomo katika mgodi huo kujifunza kutoka kwa raia wa Kichina namna bora ya uchimbaji na uendeshaji wa migodi ya dhahabu ili hata wakiondoka waweze kuendeleza mgodi huo au kuanzisha migodi mingine kwa urahisi.

Kanali Mtambi amewataka wananchi na viongozi wa Kata ya Butiama na Kijiji cha Rwamkoma kuwapokea wawekezaji hao na wengine watakaojitokeza kuwekeza katika maeneo hayo na kuishi nao vizuri ili kuwavutia wawekezaji zaidi kuja katika Mkoa wa Mara.

“Wawekezaji hawa wanamanufaa makubwa sio tu kwa Serikali kukusanya kodi bali pia wanaweza kuongeza nafasi za ajira rasmi na zisizo rasmi, kukuza biashara nyingine na kuboresha huduma za jamii katika eneo hili” amesema Mhe. Mtambi.

Akiwa katika eneo hilo, Mhe. Mtambi amepokea taraifa ya mgodi huo, amekagua maeneo mbalimbali ya mgodi huo na kuzungumza na wananchi kabla ya kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa shughuli za uchimbaji katika mgodi huo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mtambi pia na msafara wake walishiriki ibada na zoezi la kuaga mwili wa marehemu Mathias Marwa Chuchu aliyekuwa mchimbaji wa madini katika Mgodi wa IRASANILO unaomilikiwa na wachimbaji wadogo.

Aidha, Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wazazi na walezi kupeleka watoto shuleni na wananchi kuahakikisha wanawake wajawazito wanahudhuria kliniki na kutumia mfumo wa M-MAMA ili kuwarahisishia wanawake wajawazito na watoto wachanga wanaougua kwenda hospitali.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • TISEZA yahamasisha uwekezaji katika fursa za Mkoa wa Mara

    January 24, 2026
  • Mtambi afanya ziara Butiama

    January 20, 2026
  • Kanali Mtambi ahimiza upandaji miti

    January 14, 2026
  • RC Mara ateta na Viongozi wa Dini

    January 13, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa