• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TISEZA yahamasisha uwekezaji katika fursa za Mkoa wa Mara

Posted on: January 24th, 2026

Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) leo tarehe 24 Januari, 2026 imeanza ziara katika Mkoa wa Mara kwa ajili ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Mara na kutembelea miradi ya ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba na Hoteli katika Manispaa ya Musoma.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya TISEZA Balozi Dkt. Aziz Mlima amesema wapo katika Mkoa wa Mara kuendelea na kampeni maalum ya kuhamasisha uwekezaji katika fursa mbalimbali zilizopo katika Mikoa na Mara ni Mkoa wa pili baada ya kampeni hiyo kuzinduliwa rasmi katika Mkoa wa Geita hivi karibuni.

“Ninashukuru hapa (kwenye eneo la ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba) ninaona Serikali imehamasisha wadau wengi kuwekeza na taasisi za kifedha zimewaunga mkono na kwa kuwapa mikopo ya kufanikisha miradi yao” amesema Balozi Mlima.

Balozi Mlima amesema Kampeni hii inalengo kubadili fikra na mtazamo uliopo miungoni mwa watanzania kuwa uwekezaji ni mahususi kwa ajili ya raia na makampuni ya kigeni na kuwahamasisha mwamko wa wananchi kuwekeza na kuongeza idadi ya wawekezaji wa ndani katika sekta mbalimbali.

Balozi Mlima amesema Kampeni hii inawalenga makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo vijana, wajasiriamali wadogo na wakati, wafanyabiashara, waandishi wa habari na Maafisa wanaosimamia Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika Sekretarieti za Mikoa na Halmashauri zote hapa nchini.

Balozi Mlima amesema kampeni hiyo itaanzisha madawati ya uwekezaji katika mikoa na Halmashauri na kuwataka waandishi wa habari kuwa mabalozi wa kufanikisha kampeni hiyo kwa kuandika kwa usahihi taarifa zinazotolewa kuhusiana na kampeni hiyo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Uhamasishaji Uwekezaji TISEZA Ndugu Geore Mukono amesema  kuwa kampeni hiyo itaonyesha fursa mbalimbali zilizopo katika mikoa, taratibu za usajili wa miradi ya uwekezaji kwa lengo la kupata vyeti vya uwekezaji na leseni katika maeneo maalum ya kiuchumi, vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi vinavyotolewa kwa wawekezaji hapa nchini.

Ndugu Mukono amesema wawekezaji watakaojisajiri watakapa unafuu wa ushuru wa forodha hadi asilimia 100 na msamaha wa kodi hadi asilimia 75 katika vifaa vinavyotumika katika uwekezaji baada ya mradi husika kusajiliwa.

Ndugu Mukono ametolea mfano wawekezaji katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba wanaweza kupata msamaha wa kodi hadi asilimia 75 katika ununuzi wa maboti, injini, ndoano, magari ya kusafirishia samaki, vizimba, neti na kadhalika.

Kwa upande wake, Mwekezaji wa Hoteli mpya katika Manispaa ya Musoma Dkt. Felix Kivuyo amesema tangu amepata wazo la kufanya uwekezaji amepata ushirikiano kutoka kwa viongozi na watendaji wa Serikali na taasisi za kifedha ambazo zimemsaidia kutekeleza ndoto yake.

“Katika uwekezaji huu, nimefanikiwa kukutana na viongozi na watendaji mbalimbali ambao wamenipa ushirikiano mkubwa na nimefanikiwa kupata mkopo kutoka benki za CRDB na NMB” amesema Dkt. Kivuyo.

Dkt. Kivuyo amesema awali alikuwa mtumishi kwa sasa amestaafu na alianza kuwekeza katika mradi huo mwaka 2022 na kwa sasa wapo katika hatua za ukamilishaji na hoteli hiyo itakuwa na vyumba vya kulala 21, ukumbi wa mikutano, mgahawa, bar na sehemu ya nje na inategemea kuajiri watumishi wakudumu 36 na watumishi wa muda 54.

Dkt. Kivuyo ameishukuru TISEZA kwa kuanzisha kampeni hii yenye lengo la kuendelea kutoa elimu na kuwahamasisha watu wengi zaidi kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Ndugu Gambaless Timotheo amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wamefanya uhamasishaji mkubwa wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

Ndugu Gambales amesema kuwa Watumishi Mara Amcos ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara iliitikia wito wa Serikali na kuandaa andiko ambalo lilipata ufadhili wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba.

“Kwa sasa Watumishi Mara Amcos inavizimba vinne na tayari imeshavuna samaki katika msimu wa kwanza na matarajio ni kuongeza vizimba zaidi kwa kushirikiana na taasisi za kifedha” amesema Ndugu Timotheo.

Ndugu Timotheo amesema changamoto kubwa wanayoipata katika mradi huo ni upatikanaji na gharama za chakula cha samaki na kuongeza kuwa kwa sasa chakula kinatoka nje ya nchi na gharama zake ni kubwa kwa kuwa zinaunganishwa na gharama za kusafirisha chakula na mawakala wa kuuza chakula hiyo kuwa ni wachache.

Kwa upande wake, Msimamizi wa mradi wa mradi wa Rusaso General Supply Limited Ndugu Charles Makoye amesema kampuni yao ina vizimba 25 kwa sasa na kati ya hiyo 18 vinasamaki na vingine havina samaki kwa sasa.

Ndugu Makoye amesema soko la samaki lipo vizuri na kampuni yao kwa sasa inachangamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula cha samaki, uhaba na ubora wa vizimba na nyavu imara zinazoweza kuhimili ufugaji kwa muda mrefu.

“Kampuni yetu katika mpango wa baadaye inatarajia kuanzisha kiwanda cha chakula cha samaki ili kukabiliana na uhaba wa upatikanaji wa chakula cha samaki katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa” amesema Ndugu Makoye.

Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani imeanza tarehe 18 Januari, 2026 hadi tarehe 09 Aprili, 2026 itaendeshwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na imeanza kutekelezwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa na Kauli mbiu ”Unawezeshwa Kuwekeza kwa kupewa Unafuu wa Mtaji”

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • TISEZA yahamasisha uwekezaji katika fursa za Mkoa wa Mara

    January 24, 2026
  • Mtambi afanya ziara Butiama

    January 20, 2026
  • Kanali Mtambi ahimiza upandaji miti

    January 14, 2026
  • RC Mara ateta na Viongozi wa Dini

    January 13, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa