Tanzania inamiliki asilimia 51 ya eneo la Ziwa Victoria ambayo ni sawa na Kilomita za mraba 35, 088. Aidha Mkoa wa Mara unamiliki Kilomita za mraba 9,825 sawa na asilimia 28 ya sehemu ya umiliki wa Tanzania. Wilaya zinazopakana na Ziwa kwa upande wa Mkoa wa Mara ni Bunda, Butiama, Musoma na Rorya. Uwepo wa Ziwa Victoria umechangia sana kutokana na mazao ya samaki kutumika kwa matumizi ya chakula kwa binadamu na mifugo.
AJIRA ZITOKANAZO NA SEKTA YA UVUVI.
Sekta ya uvuvi inatoa ajira ya moja kwa moja (direct employment) kwa wavuvi na ajira isiyo ya moja kwa moja (indirect employment) kwa wadau wengine. Mwaka 2014 sekta ya uvuvi Mkoa wa Mara imetoa ajira kwa wavuvi 24,220 hii ni pungufu ya wavuvi 1,158 ikilinganishwa na wavuvi 25,378 mwaka 2012. Upungufu huu pamoja na mambo mengine unatokana na kupungua kwa rasilimali ya sekta ya uvuvi. Aidha kutokana na utafiti wa shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) mvuvi mmoja anatoa ajira kwa watu angalau 4 (kama vile, wachakataji wa samaki, wachuuzi na wafanya biashara ya samaki, wamiliki wa vyombo vya uvuvi, mafundi boti, washona nyavu na wauzaji wa zana za uvuvi, mama lishe n.k.). kwa mantiki hii sekta ilitoa ajira pia kwa wadau wengine wasiopungua 96,880 kwa mwaka 2014.
WASTANI WA UVUNAJI WA SAMAKI
Kwa mwaka 2015/2016 zilivuliwa tani 21,241.139 za samaki wenye thamani ya Shilingi 96,988,512,313 pesa hizi ni mapato ya wavuvi.
Wamiliki wa viwanda vya samaki (Musoma Fish na Prime Catch) kwa mwaka 2015/2016 wamepata Shilingi 45,793,965,671.87 kutokana na mauzo ya Kilogramu 2,765,753 za samaki na mazao yake nje ya Nchi na kulipa Mrabaha wa Shilingi 834,274,048. Aidha wasafirishaji wadogo wa samaki na mazao yake walipata jumla yaShilingi 105,214,740 kwa mauzo ya kilo 297,425 za dagaa, furu na unga wa Samaki katika soko la Nchi ya Kenya. Kwa upande wa Serikali kuu na Halmashauri za Wilaya na Manispaa zilipata jumla ya Shilingi 1,910,607,617 kutokana na ada na tozo mbalimbali za shughuli za uvuvi ( Serikali kuu Tshs. 955,918,403 na Halmashauri Tshs. 954,689,214.
MIALO YA SAMAKI
Kwa mujibu wa sensa ya uvuvi 2014, Mkoa una jumla ya mialo 174 ambapo mialo 172 inasimamiwa na vikundi vya wadau wa uvuvi (BMUs). Mialo yenye vibanda / majengo ya kupokelea samaki ni 17. Aidha, mialo 99 ina huduma za afya (healthy clincs), mialo 131 ina shule za msingi, mialo 30 ina vyoo vya umma, mialo 165 ina huduma za benki , mialo 6 ina huduma ya umeme na mialo 79 inafikika kwa barabara wakati wowote. Sambamba na kutegemea Ziwa Victoria Sekta ya Uvuvi imekuwa ikikua kwa kasi kubwa kwani hadi kufikia Mwezi Desemba 2016, jumla ya mabwawa 319, vizimba 58 na malambo / mabwawa ya asili 72 (malambo 24 ni ya kudumu na yana samaki) yenye samaki aina ya Sato (Oreochromis sp.) na Kambale (Clarius sp).
Mkoa wa Mara umeendelea kusimamia ipasavyo Sera ya uvuvi ya mwaka 1997 kwa ajili ya kulinda, kuendeleza, kukuza usimamizi endelevu wa rasilimali ya uvuvi kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo. Jukumu hili ni zito na linahitaji ushiriki wa jamii mpana zaidi kama ililivyo ainishwa katika kifungu cha 25 (I) cha kanuni za uvuvi 2009.
Katika kutekeleza majukumu na usimamizi wa Sheria za Uvuvi kwa kipindi cha Julai 2016 hadi April 2017 Mkoa umeweza kukamata Zana Haramu na Wavuvi kama ifuatavyo:- Makokoro ya Sangara 1,113, Nyavu za Utali 9,346, nyavu za Dagaa 676, Kamba za Makokoro mita 169,896, Nyavu ndogo chini ya Inchi 6 4,454, Mitumbwi 87, Sangara wachanga 22,807 Kgs, Sato wachanga 342, Injini 2, Samaki wenye sumu 48.5, Nyavu za kuunganisha 332 Kgs huku Watuhumiwa 98 wakifikishwa Mahakamani na Watuhumiwa 71 walilipa faini na kupatikana jumla ya Shilingi 6,435,000. Kutokana na usimamizi mzuri wa rasilimali za samaki kwa sasa kuna ongezeko kubwa la samaki kutokana na kupungua kwa vitendo vya uvuvi haramu.
Jedwali Na. 9: Taarifa ya utekelezaji wa shughuli za Doria mwezi Julai, 2016 hadi Aprili, 2017
WILAYA |
MAKOKORO YA SANGARA |
NYAVU ZA UTALII |
DAGAA NET |
KAMBA ZA KOKORO (M) |
NYAVU NDOGO<6” |
MITUMBWI |
WATUHUMIWA |
SANGARA WACHANGA (KG) |
SATO WACHANGA |
INJINI |
FAINI |
SAMAKI WA SUMU (Kgs) |
NYAVU ZA KUUNGANISHA |
|||||
WALIOLIPISHWA FAINI |
WALIOFUNGULIWA MAHAKAMANINIANI |
|||||||||||||||||
MUSOMA |
144 |
741 |
29 |
37,533 |
1,698 |
61 |
53 |
52 |
8,361 |
0 |
2 |
6,435,000 |
30 |
82 |
||||
RORYA |
45 |
995 |
24 |
9,700 |
253 |
20 |
7 |
0 |
45 |
15 |
0 |
0 |
250 |
|||||
BUTIAMA |
21 |
78 |
4 |
3,552 |
20 |
6 |
1 |
3 |
1,000 |
0 |
0 |
0 |
0 |
|||||
BUNDA |
26 |
0 |
0 |
12,800 |
60 |
0 |
6 |
0 |
100 |
300 |
0 |
0 |
0 |
|||||
TARIME |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
0 |
400 |
0 |
0 |
18.5 |
0 |
|||||
JUMLA |
236 |
1,787 |
57 |
63,585 |
2,031 |
87 |
67 |
55 |
9,906 |
315 |
2 |
48.5 |
332 |
|||||
HALMASHAURI YA WILAYA YA MUSOMA |
||||||||||||||||||
|
178 |
904 |
273 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
||||
NYAVU ZILIZOTEKETEZWA |
||||||||||||||||||
|
149 |
2,564 |
24 |
78,674 |
150 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
||||
NYAVU AMBAZO HAZIJATEKETEZWA |
||||||||||||||||||
|
11 |
6 |
- |
611 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
||||
JUMLA |
338 |
3,476 |
297 |
79,285 |
150 |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
- |
||||
HALMASHAURI YA WILAYA YA RORYA |
||||||||||||||||||
|
165 |
3,213 |
199 |
826 |
4 |
- |
- |
5 |
53 |
27 |
- |
- |
- |
- |
||||
HALMASHAURI YA WILAYA YA BUNDA DC |
||||||||||||||||||
|
337 |
823 |
28 |
26,200 |
739 |
- |
4 |
3 |
7,800 |
- |
- |
- |
- |
- |
||||
HALMASHAURI YA MJI WA BUNDA |
||||||||||||||||||
|
37 |
47 |
95 |
- |
1,530 |
- |
- |
35 |
5,048 |
- |
- |
- |
- |
- |
||||
JUMLA KUU |
1,113 |
9,346 |
676 |
169,896 |
4,454 |
87 |
71 |
98 |
22,807 |
342 |
2 |
- |
48.5 |
332 |
||||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, 2017
CHANGAMOTO
MIKAKATI
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa