Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 yalionesha kuwa Mkoa, ulikuwa na idadi ya wakazi 1,743,830 ambao wanaongezeka kwa asilimia 2.5 kwa mwaka. Hivyo, kwa maoteo ya idadi ya watu hadi Desemba 31, 2017 Mkoa unakadiriwa kuwa na watu wapatao 1,989,134. Kutokana na makadirio hayo, mahitaji ya chakula kwa mwaka 2017 yanakadiriwa kuwa tani 544,525 za mazao ya nafaka na mikunde.
UTEKELEZAJI WA MALENGO YA KILIMO KWA MWAKA 2016/2017
Katika msimu wa kilimo 2016/2017, Mkoa ulikuwa na lengo la kulima jumla ya hekta 453,830 kwa lengo la kuvuna tani 1,008,649 za mazao ya chakula mchanganyiko. Kati ya hizo mazao ya wanga ni hekta 419,801 kwa lengo la kuvuna tani 972,879 na mikunde hekta 34,029 kwa lengo la kuvuna tani 35,770. Utekelezaji wa malengo ya kilimo cha mazao ya chakula mchanganyiko katika msimu wa vuli 2016/2017 unakadiriwa kufikia hekta 118,005 sawa na asilimia 42% ya lengo lililowekwa la Hekta 279,633 na makadirio ya mavuno kuwa tani 193,060 sawa na 24%, ikilinganishwa na lengo la tani 790,377 msimu wa vuli.
Jedwali Na. 8: Malengo ya kilimo na utekelezaji kwa mazao ya chakula katika msimu wa vuli 2016/2017
Aina ya Mazao
|
MALENGO |
UTEKELEZAJI |
%ya utekelezaji
|
|||
HA |
TANI |
HA |
TANI |
HA |
TANI |
|
Mazao ya Wanga
|
259,109.7 |
760,149.55 |
109,344.29 |
190,037.39 |
42 |
25 |
Mazao ya Mikunde
|
20,523.3 |
30,227.45 |
8,660.83 |
3,022.75 |
42 |
10 |
JUMLA
|
279,633 |
790,377 |
118,005.12 |
193,060.14 |
42 |
24 |
Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 2017
Katika Msimu wa masika 2016/2017, Mkoa umejiwekea lengo la kulima jumla ya Ha.335,824.88 kwa lengo la kuvuna tani 815,588.86 kwa mazao ya chakula mchanganyiko. Kulingana na hali ya hewa katika kipindi cha Masika kuwa ni ya kuridhisha kwa maeneo mengi Mkoa unatarajia kupata mavuno ya kutosheleza ambapo mazao mengi yapo katika hatua mbalimbali za kukomaa. Kwa ujumla, hali ya chakula bado kinapatikana ndani ya Mkoa hususan katika maduka, masoko / magulio ya vijiji, kata na maeneo ya baadhi ya Wilaya yameanza kuvuna mazao aina ya nafaka katika msimu wa vuli 2016/2017 kama vile Wilaya za Tarime na Serengeti
UENDELEZAJI WA KILIMO CHA UMWAGILIAJI
Eneo la Mkoa linaloweza kumwagiliwa (Irrigation Development Potential) ni hekta 910,000, kati ya hizo uwezo wa juu (High potential) ni 210,100 Ha, uwezo wa kati (Medium potential) ni 576,500 Ha na uwezo wa chini (Low Potential) ni 123, 400 Ha. Jumla ya hekta 4,600 sawa na asilimia 2.2 ya eneo la uwezo wa juu (High potential 210,100 Ha) ndizo zinaendelezwa kwa kilimo cha Umwagiliaji. Kati ya hizo hekta 1,926 zimejengewa miundombinu bora na hekta 2,764 zinaendelezwa kwenye maeneo yasiyojengewa miundombinu bora ya umwagiliaji.
Baadhi ya maeneo yaliyoanza utekelezaji kwa kufanyiwa usanifu / kujengewa miundombinu ya Umwagiliaji ni bonde la Nyakunguru (katika Wilaya ya Tarime), Bonde la Mto Mara chini ya mradi wa NBI/NELSAP, Ochuna, Rabuor, Chereche, Baraki “Sisters Farm’’, Chereche Singida, Irienyi (katika Wilaya ya Rorya), Mesaga, Bugerera, Kenyamonta, Nyamitita (Katika Wilaya ya Serengeti), Buswahili, Butiama (Wilaya ya Butiama), Masinono, Maneke, Chirorwe (Wilaya ya Musoma), Nansimo, Maliwanda, Nyatwali, Namuhula, Kisangwa na Bonde la Suguti (Wilaya ya Bunda). Miradi yote hii iko katika hatua mbali mbali za utekelezaji
HUDUMA ZA UGANI
Kwa kipindi cha mwaka (2010/2011 - 2015/2016) pamekuwapo jitihada ya kuongeza wataalam wa kilimo ndani ya Mkoa, ingawa lengo halijafikiwa. Lengo ni kila kijiji kupata mtalaam wa ugani mwenye fani ya kilimo sambamba na Makao Makuu ya Mkoa / Wilaya watakaoweza kushughulikia masuala mtambuka katika kilimo kama vile Pembejeo, mazao ya biashara n.k. Hadi kufikia Desemba 2016, Mkoa ulikuwa na upungufu wa Wagani 197 katika ya mahitaji ya Wagani 628 kwa ajili ya kuhuduma maeneo hasa ya Vijiji na Kata.
PEMBEJEO NA ZANA ZA KILIMO
Katika msimu 2016/2017, Mkoa wa Mara umegawiwa Pembejeo zenye ruzuku ya tani 100 za mbolea ya kukuzia (Urea) na tani 50 ya mbegu za mahindi zenye jumla ya thamani ya Tshs. 319,500,000.00. Hata hivyo, Mkoa haukupata mbolea ya kupandia wala mbegu za Mpunga. Aidha, kulingana na mwongozo wa Pembejeo msimu 2016/2017 umeelekeza kamati za Pembejeo za Mikoa kutoa kipaumbele cha mgao kwenye maeneo yenye miundombinu ya umwagiliaji iliyokamilika. Jumla ya wakulima 5,000 watanufaika na mbegu za mahindi ambapo wakulima 2,000 watanufaika na mbolea ya kukuzia. Matumizi ya Zana bora za kilimo yanaongezeka na hivyo, matumizi ya jembe la mkono yanapungua japo sio kwa kiasi kikubwa. Wakulima wanaotumia wanyama kazi kwa kulimia ni asilimia 37.08, wanaotumia Matrekta ni asilimia 4.75 na jembe la mkono hutumika kwa asilimia 58.17.
CHANGAMOTO ZA JUMLA ZA SEKTA YA KILIMO
MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa