• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Wananchi Mara wahimizwa kupiga kura kwa amani na utulivu

Posted on: October 25th, 2025

Wananchi wa Mkoa wa Mara wakishirikiana na Kikundi cha Jogging Musoma leo tarehe 25 Oktoba, 2025 wamekimbia mbio za pole kwa lengo la kuhamasisha wananchi kufanya mazoezi, kupima afya zao na kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Akizungumza katika viwanja vya Hospitali ya Manispaa ya Musoma wakati wa kuhitimisha mbio hizo, Mwenyekiti wa Kikundi cha Jogging Musoma Ndugu Daudi Yunge amesema Kikundi hicho kinawashukuru wananchi wengi waliojitokeza kushiriki mbio hizo na kuwataka kuendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya zao.

Ndugu Yunge amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kushiriki mbio hizo ambazo zinalenga pamoja na mambo mengine kuipongeza Serikali kwa kazi nzuri iliyofanyika katika kuboresha afya za wananchi wa Mkoa wa Mara na hususan katika ujenzi wa miundombinu, upatikanaji wa vifaa tiba na dawa pamoja na ongezeko la huduma za afya.

“Mambo mengi na makubwa yamefanyika katika Mkoa wa Mara katika sekta ya afya, kwa sasa huduma za matibabu ya kibingwa na bobezi yanapatikana bila ya kutakiwa kusafiri kwenda nje ya Mkoa wa Mara” amesema Ndugu Yunge.

Aidha, Ndugu Yunge amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura tarehe 29 Oktoba, 2025 ili kuwachagua viongozi watakaoyaendeleza miradi mikubwa iliyofanyika katika Mkoa wa Mara kwa kipindi kingine cha miaka mitano.  

Akizungumza wakati wa kuhitimisha shughuli hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka ambaye amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi katika tukio hilo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa kushiriki uchaguzi kwa amani na utulivu.

Mhe. Chikoka amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mara uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu na kuwataka wananchi kuondoa hofu kwa kuwa Serikali ya Mkoa wa Mara imejipanga kulinda amani iliyopo wakati na baada ya uchaguzi mkuu.

“Serikali ya Mkoa wa Mara imejipanga kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu na hamna atakayeanzisha vurugu wala maandamano, tujitokeze tutimize haki yetu ya kikatiba ya kuwachagua viongozi” amesema Mhe. Chokoka.

Mhe. Chikoka amewakumbusha wananchi kuhusiana na mambo mengi ambayo yamefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa wakati wa uongozi wake wa miaka minne na kuwataka kuwachagua viongozi wanaoona wanaweza kuleta maendeleo kama hayo.

Aidha, Mhe. Chikoka ametumia fursa hiyo kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi ya viungo mara kwa mara kwa kuwa pamoja na faida zake kiafya ya binadamu, mazoezi yanaboresha mtandao wa marafiki katika jamii.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu amekishukuru kikundi cha Jogging Musoma kwa kuandaa mbio hizo na kuishirikisha Serikali ya Mkoa wa Mara katika tukio hilo ambalo linalenga kuimarisha afya za wananchi kwa kufanya mazoezi, kushiriki kupima afya zao na kufanya usafi.

Dkt. Masatu amesema mazoezi ni muhimu katika afya ya binadamu na hususan kwa ajili ya kuzuia na kupunguza athari za magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo kwa sasa yameshamiri katika jamii kutokana na mitindo wa maisha na aina za vyakula na hivyo amekishukuru kikundi hicho kwa kuwakumbusha wananchi kwa vitendo.

Kauli mbiu ya shughuli hiyo ilikuwa Kimbia kwa Afya, Tembea kwa Amani, Jitokeze Kupiga Kura 2025 ikiwahamasisha wananchi kushiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika hapa nchini Jumatano ijayo ya tarehe 29 Oktoba, 2025.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wananchi Mara wahimizwa kupiga kura kwa amani na utulivu

    October 25, 2025
  • Mtambi awataka wakulima Bunda na Musoma kuchangamkia fursa ya kilimo cha choroko

    October 24, 2025
  • Kusaya: wataalamu wa kilimo fanikisheni Mpango wa Mageuzi ya Kilimo 2050

    October 24, 2025
  • Demokrasia inaendelea kupevuka katika Mkoa wa Mara: Mtambi

    October 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa