• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Serikali yaipongeza Mara kwa mabadiliko

Posted on: December 24th, 2025

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi leo tarehe 22 Disemba, 2025 amefanya ziara katika Mkoa wa Mara na kuupongeza Mkoa wa Mara kwa mabadiliko makubwa yaliyofanikisha wanawake wanne kuchaguliwa kuwa wabunge wa majimbo katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Mhe. Mahundi anasema kwa historia, mila na tamaduni za wananchi wa Mkoa wa Mara zilizozoeleka isingekuwa rahisi, kuwachagua wanawake katika nafasi ya ubunge wa jimbo, jambo kubwa linalohitaji kupongezwa na wadau wote wa maendeleo.

“Ninaimani mabadiliko haya yanaweza kuwa yamechochewa na uimara aliouonyesha Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuiongoza Serikali kutekeleza miradi kwa ufanisi mkubwa” amesema Mhe. Mahundi na kuongeza kuwa nafasi aliyonayo sio ya upendeleo ila imetokana na uimara wake.

Mhe. Mahundi ameupongeza uongozi wa Serikali katika Mkoa wa Mara na Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara kwa kufanikisha mabadiliko hayo kuweza kutokea katika Mkoa wa Mara na kuwataka viongozi wote kuwasaidia wabunge hao kutekeleza majukumu yao kiufanisi ili kuhamasisha wanawake wengi zaidi kupewa nafasi za uongozi.

Akizungumza wakati wa mapokezi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na CCM Mkoa wa Mara, Mhe. Mahundi amesema Mkoa wa Mara unakuwa mfano wa kuigwa katika mabadiliko kwa vitendo kutoka katika mazoea, mila na tamaduni zinazokwamisha maendeleo kwenda katika maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amesema katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 wananchi wa Mkoa wa Mara wameamua kwa mara ya kwanza katika historia kuwapa ubunge wa majimbo wanawake wanne kati na nafasi 10 zilizokuwa zinagombaniwa.

“Mkoa wa Mara tumeweza kufika asilimia 40/60 kwa mara ya kwanza. Hii inatokana na jitihada mbalimbali zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau kuwahamasisha wananchi kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi wa Mkoa wa Mara kwa kushiriki uchaguzi mkuu kwa wingi bila kufanya vurugu kutokana na kuweka maendeleo kama kipaumbele chao cha kwanza.

Wabunge wanawake waliochaguliwa katika Mkoa wa Mara ni pamoja na Mhe. Migore Miraji Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini; Mhe. Mary Daniel Mbunge wa Jimbo la Serengeti, Mhe. Esta Matiko Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini na Mhe. Esta Bulaya Mbunge wa Jimbo la Bunda. 

Hii ni mara ya kwanza kwa Mkoa wa Mara kupata nafasi nyingi za wabunge wanne wanawake kupitia majimbo ya uchaguzi.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Nyansaho ateta na Wazee wa Mara

    December 24, 2025
  • Mtambi: Mara imejipanga kuhakikisha usalama wakati wa sikukuu

    December 24, 2025
  • Serikali yaipongeza Mara kwa mabadiliko

    December 24, 2025
  • Mtambi aomba kupandishwa hadhi kwa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare

    December 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa