• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi aomba kupandishwa hadhi kwa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare

Posted on: December 24th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 22 Disemba, 2025 amempokea na kuzungumza na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi na kuongelea umuhimu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kupandishwa hadhi na kuanza kutoa programu za Shahada.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mhe. Mtambi amesema Chuo hicho kimekuwa na programu za cheti na Diploma kwa muda mrefu na kutokana na mabadiliko yanayoendelea katika sekta mbalimbali nchini ni muhimu sana Taifa lipate wataalamu wengi wa Maendeleo ya Jamii ili kutafsiri dhana ya maendeleo kwa wananchi.

“Sasa hivi mambo mengi yanaenda kisayasi na ni muhimu sana kama wataalamu wa Maendeleo ya Jamii  kuwa na ubobevu mkubwa wa kuweza kutafsiri fursa zilizopo katika sekta mbalimbali ili ziweze kuleta tija kwa wananchi” amesema Mhe. Mtambi. 

Mhe. Mtambi amesema kwa sasa wananchi wameanza kupambana kupata maendeleo yao hivyo ni muhimu kuwa na wataalamu wengi wa Maendeleo ya Jamii ambao watawasaidia wananchi kufikia malengo ya maendeleo yaliyowekwa kitaifa na kimataifa.

Kanali Mtambi amesema Maendeleo ya Jamii inagusa maendeleo ya sekta zote za katika jamii na hivyo kuwa na wataalamu wenye elimu ya umahiri na ubobevu ni muhimu sana kwani ndio watakaoishauri  Serikali kuhusiana mwelekeo sahihi wa maendeleo ya Taifa.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi MaryPrisca Mahundi amesema tayari Serikali imefikiria kuhusu kukipandisha hadi Chuo hicho na mchakato wake umeanza na unaenda vizuri.

Akizungumza kwa nyakati tofauti tofauti Mhe. Mahundi amesema mchakato wa kukipandisha hadhi Chuo hicho unaendelea vizuri na kama Wizara wanaendelea kulisukuma jambo hilo ili Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kipandishwe hadhi na kuanza kutoa Shahada mbalimbali.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mhe. Migore Miraji amesema Chuo hicho kwa sasa kina miaka 57 tangu kilipoanzishwa na muda wote huo kinatoa programu mbalimbali za Cheti na Diploma na kuongeza kuwa kwa sasa kinahitaji kubadilika ili kuwasaidia zaidi wananchi.

Mhe. Miraji amesema kuwa Chuo kina miundombinu ya kutosha na kama itahitajika kuongeza haitahitaji uwekezaji mkubwa sana ikilinganishwa na kuanzisha Chuo kipya na kikianza kutoa shahada kitawasaidia wanafunzi wanaotoka Mkoa wa Mara kupata elimu ya juu jirani na makazi yao.   

Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Mhe. Alex Mtaki Nyambiti amesema Halmashauri ya Manispaa ya Musoma inatengemea kuwa Chuo hiki kikipandishwa hadhi kitaisaidia  katika kuchechemua uchumi wa wananchi wa Manispaa hiyo na kupandisha makusanyo ya Halmashauri.

“Kwa sasa mapato ya ndani ya Manispaa ya Musoma sio makubwa ikilinganishwa na mahitaji ya mikopo kutoka katika vikundi vinavyotarajiwa kunufaika na mikopo hiyo” amesema Mhe. Nyambiti na kuongeza kuwa katika kupandisha mapato Halmashauri hiyo inategemea Chuo hicho, uvuvi na biashara zilizopo katika Manispaa hiyo.

Mhe. Nyambiti amesema makusanyo ya Halmashauri yakiongezeka, itaongeza wigo wa mikopo ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu jambo ambalo litasaidia kupunguza tatizo la makusanyo hafifu na mikopo kidogo inayotolewa na Manispaa hiyo kwa wananchi.  

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare Ndugu Paschal Mahinyila amesema Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kimeanzisha mchakato wa kujiunga na Taasisi ya Maendeleo ya Jamii Tengeru na kwa msaada wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum mchakato huo unategemewa kukamilika ndani ya miezi sita ijayo.

Ndugu Mahinyila amesema kuwa mchakato huo ukikamilika, Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare kitakuwa sehemu ya Taasisi ya Tengeru na kinategemea kuanza kutoa Shahada mbalimbali za Maendeleo ya Jamii kuanzia mwaka wa masomo 2026/2027 na kuboresha miundombinu ya Chuo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa jengo la utawala, mabweni na madarasa. 

Ndugu Mahinyila amesema kwa sasa Chuo kina wanafunzi 905 na kati yao 313 ni wanaume wakati wanafunzi 592 ni wanawake na kina watumishi 26 walioajiriwa na watumishi wa kujitolewa ambao ni wakufunzi watatu.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mahundi baada ya kupokelewa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ametembelea ofisi za Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, ametembelea ofisi za wamachinga Mkoa wa Mara, kutembelea Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare na baadaye kuzungumza na wajasiriamali wa Mkoa wa Mara katika ukumbi wa MCC.

 Akiwa katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare, Mhe. Mahundi amepokea taarifa ya Chuo, amefungua mdahalo wa Maadili na Uzalendo na kuwahimiza wanachuo kuwa wazalendo na kuipenda, kuilinda na kuitetea Tanzania wakati wote.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Nyansaho ateta na Wazee wa Mara

    December 24, 2025
  • Mtambi: Mara imejipanga kuhakikisha usalama wakati wa sikukuu

    December 24, 2025
  • Serikali yaipongeza Mara kwa mabadiliko

    December 24, 2025
  • Mtambi aomba kupandishwa hadhi kwa Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare

    December 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa