• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Afya

HUDUMA ZA AFYA MKOA WA MARA

Vituo vya Kutolea Huduma za Afya: Mkoani Mara Zahanati zimeongezeka kutoka 221 mwaka 2010 hadi 241 mwaka 2015 kati ya hizo 26 ni za mashirika ya dini na 27 ni za watu binafsi sawa na ongezeko la asilimia 9. Vituo vya afya vimeongezeka kutoka 36 mwaka 2010 hadi 41 mwaka 2015 ambapo 6 ni vya mashirika ya dini na 7 sekta binafsi sawa na ongezeko la asilimia 13. Mkoa wa Mara unatekeleza mpango wa maendeleo wa afya ya msingi (MMAM) tangu mwaka 2007. Hadi kufikia mwaka 2015 Mkoa umetumia Tsh. 4,369,742,665/= na umeweza kujenga Zahanati 50, Vituo vya Afya 3,Nyumba za watumishi 33 na kukarabati Zahanati 91, Vituo vya Afya 18 na nyumba za watumishi 37. Bado mkoa haujafikia lengo ambapo hadi kufikia 2015, Mkoa una jumla ya vijiji na mitaa 673, vyenye zahanati ni 241 ambayo ni asilimia 36 na Kata 171 zenye vituo vya afya ni 41 (ambayo ni asilimia 24), hii inachangiwa na ufinyu wa rasilimali fedha.


Aidha ili kuhakikisha kuwa Mkoa unakuwa na Hospitali ya rufaa yeye miundombinu, vifaa tiba na wataalam wa kutosha kutoa huduma za Kibingwa katika fani zote muhimu, Uongozi wa Mkoa umeamua kuendeleza ujenzi wa jengo la hospitali ya Kwangwa ili iwe Hospitali ya rufaa ya Mkoa itakayoitwa Mwalimu Nyerere Medical Centre. Kuanzia mwaka 2012/2013 hadi 2013/2014 – Serikali ilitenga kiasi cha shilingi 4.2 bilioni na pia kutenga kiasi cha shilingi 2.1 bilioni mwaka 2014/2015. Hadi sasa mkoa umepokea jumla ya Tsh 3,334,967,000 katika bajeti ya serikali kwa ajili ya mradi huu kwa mwaka 2012/2013 na 2013/2014 .Kazi zilizofanyika 2014/2015 ni pamoja na:-

  • Kuwalipa fidia wananchi waliopisha eneo hilo wapatao 62 waliokuwa wanadai Jumla ya Tsh 501,658,413.
  • Ujenzi wa Awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali hii inagharimu Tsh 2,873,607,300.1; ujenzi umeanza na muda wa kukamilisha ni mwaka 1 kuanzia tarehe 17/04/2014 hadi tarehe 17/04/2015. Aidha jumla ya Tsh 1,299,177,712.30 zimeshalipwa (Mkandarasi Tsh 1,175,526,682 na mshauri mwelekezi Tsh 123,651,029.60).
  • Ujenzi wa uzio kuzunguka eneo lote la kiwanja inaendelea kwa gharama ya Tsh 264,919,395.50.

Mwonekano wa Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere 

Watumishi wa afya wa Serikali katika Mkoa wameongezeka toka 1,307 mwaka 2010 hadi 2424 mwaka 2015 sawa na ongezeko la asilimia 85.5 Kwa mfano Madaktari bingwa mwaka 2010 walikuwa 3 na mwaka 2015 wako 8, Wauguzi wenye shahada (BSc Nursing) mwaka 2010 hawakuwepo na mwaka 2015 wako 18 na Madaktari (MD) mwaka 2010 walikuwa 10 na mwaka 2015 wako 23.

Bado kuna changamoto ya upungufu wa watumishi, kwani waliopo ni asilimia 65 tu ya mahitaji. Sababu za upungufuu huu ni watumishi kutopenda kuja Mkoa wa Mara na wanaokuja huhama baada ya muda mfupi. Katika kukabiliana na tatizo hili Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri unatumia mbinu na mikakati mbalimbali ili kuvutia watumishi kuja Mara na kuwabakiza. Mikakati hiyo ni pamoja na motisha kwa watumishi, kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuwapa stahili zao kwa wakati.

Mkakati wa Mkoa wa kuboresha Afya ya mama na mtoto kwa lengo la kupunguza vifo vya mama na mtoto
Mkoa una Mkakati wa kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga unaoendelea kutekelezwa. Lengo kuu la mkakati huu ni kupunguza vifo vya mama wajawazito kutoka 91 mwaka 2013 hadi 40 mwaka 2016. Malengo mahususi ni pamoja na:

  • Kuboresha vituo vya Afya 13 ili viweze kutoa huduma ya upasuaji na damu
  • Kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango toka asilimia 18 mwaka 2010 hadi 60 mwaka 2016.
  • Kujenga kituo cha damu salama
  • Kuhamasisha mama wajawazito wajifungulie katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
  • Kutoa mafunzo kwa watumishi wa Afya kuhusu uzazi salama.
  • Usimamizi shirikishi na mafunzo kazini.

Hadi sasa Mkoa umenunua pikipiki kwa Maafisa Tarafa kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa mkakati huu na kupata takwimu sahihi katika ngazi za vitongoji,vijiji na kata na ujenzi wa Kituo cha Damu salama cha Mkoa katika hospitali ya Mkoa umeanza .

Mafanikio yameonekana katika ongezeko la matumizi ya uzazi wa mpango, yameongezeka toka 18% mwaka 2010 hadi 40% mwaka 2015, kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za Afya imeongezeka toka 37% mwaka 2010 hadi 63% mwaka 2015.

Maboresho ya vituo 13 (Musoma Manispaa – Nyasho; Musoma DC– Murangi; Butiama DC – Kiagata; Bunda DC– Kasahunga, Ikizu na Manyamanyama; Tarime DC – Nyamongo, Muriba na Nyarwana; Rorya DC – Kinesi na Utegi; Serengeti DC – Natta na Iramba) yamekamilika kwa asilimia 95.

Vifo vya wazazi vimepungua kutoka 110/100,000 (2010) mpaka 101/100,000 (2015), kiwango cha vifo vya akinamama vitokanavyo na uzazi viko chini ukilinganisha na viwango vya kitaifa ambavyo mwaka 2010 kitaifa ilikuwa ni 578/100,000 hadi kufikia 454/100,000 mwaka 2015 kitaifa.

Mkoa umepata wadau MCSP – Jhpiego, Engenderhealth, Marie Stopes wa kushirikiana nao katika kutekeleza mkakati huu.

Huduma ya Watoto chini ya Miaka Mitano

  • Mkoa wa Mara una mikakati inayolenga kuboresha huduma ya watoto chini ya miaka mitano na kuzuia vifo. Mikakati hiyo ni pamoja na kutoa chanjo kwa watoto wote ambapo kwa sasa asilimia 98 ya watoto hupata chanjo, kuzuia ugonjwa wa malaria kwa kupuliza dawa za ukoko majumbani, kusambaza na kutumia vyandarua na kutibu sahihi ugonjwa wa malaria, pneumonia na kuharisha kwa utaratibu wa IMCI.
  • Mikakati hii imeweza kupunguza vifo vya watoto chini ya mwaka mmoja (IMR) kutoka 75/1,000 mwaka 2010 na kufikia 50/1,000 mwaka 2015 sawa na punguzo la asilimia 25. Kitaifa vifo vimepungua kutoka 62/1,000 mwaka 2010 hadi 51/1,000 mwaka 2015.
  • Vifo vya watoto chini ya miaka mitano vimepungua kutoka 109/1,000 mwaka 2010 na kufikia 54/1,000 mwaka 2015 sawa na punguzo la asilimia 46.8. Kitaifa vifo vimepungua kutoka 96/1,000 mwaka 2010 hadi 51/1,000 mwaka 2015.

 

VVU/UKIMWI
Mkoa wa Mara umefanya juhudi kubwa katika kupanbana na tatizo la VVU/UKIMWI.

Lengo kuu la Mkoa ni kutokomeza maambukizi mapya ya VVU/UKIMWI ifikapo mwaka 2016: Ili kufikia lengo hili Mkoa unatekeleza mambo yafuatayo:

  • Kuongeza Vituo vya kutolea huduma ya kuzuia maambukizi ya  VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto(PMTCT) (Vituo hivi vimeongezeka  kutoka 27 (2005) na kufikia 233(2015). Mchanganuo kiwilaya kwa mwaka 2014 ni kama ifuatavyo; Manispaa 17, Butiama 56, Tarime 32, Bunda 44, Serengeti 46 na Rorya 38. Lengo ni kufikia vituo 275 kimkoa ifikapo 2015.
  • Kuongeza vituo vya kutolea huduma ya CTC (hivi vimeongezeka kutoka 12 (2005) na kufikia 50 (2014).  Lengo ni kufikia vituo 94 ifikapo 2015. Vilevile kwa mwaka 2014 kuna vituo 10 vya huduma ya mkoba kwa ajili ya huduma ya ushauri nasaha, upimaji na utoaji dawa ambapo mwaka 2005 havikuwepo.
  • Mwaka 2014 Mkoa kwa kushirikiana na wadau unatoa huduma ya uchunguzi wa saratani ya shingo ya kizazi katika vituo vinne (Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Musoma, Hospitali ya Shirati, Bunda na Tarime).  Huduma hii ilikua haitolewi mkoani Mara mwaka 2005.
  • Vile vile huduma ya kutahiri wanaume, inaendelea kutolewa katika wilaya ya Rorya.

Mikakati hii imeweza kupunguza maambukizi ya VVU kutoka asilimia 7.7 mwaka 2007 hadi 4.5 mwaka 2012.
Upatikanaji wa Dawa na vifaa Tiba Katika kuboresha upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi muhimu kwa kipindi cha 2014/2015 Mkoa kwa kushirikiana na halmashauri, wadau wa afya (CSSC, AIDS Relief) na MSD umeunda kikosi kazi (Technical working group) ambacho kimeimarisha mawasiliano kuhusu upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi na kuhakikisha vinakuwepo kwenye vituo vya kutolea huduma muda wote. Mawasiliano hayo yameimarishwa kwa kutumia mfumo wa watsup group. Nia ni kufahamu uhaba na upatikanaji wa bidhaa ili kuweza kugawa upya bidhaa zilizopo kulingana na uhitaji. Upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitenganishi katika vituo vya kutolea huduma umeboreka kutoka asilimia 66 mwaka 2010 hadi asilimia 75 mwaka 2015.

Kuboresha Huduma za Hospitali za Mkoa na Halmashauri
Katika kuboresha utoaji huduma katika hospitali ya Mkoa mambo yafuatayo yamefanyika kwa mwaka 2014/2015;

  • Watumishi 40 wa kada Mbalimbali (madaktari 3, Afisa Muuguzi 1, Afisa wauguzi wasaidizi 4, wauguzi 4, wahudumu wa afya 19 wataalamu wa maabara 4, mfamasia 1, mteknolojia mionzi 3 na katibu wa Afya 1) wameajiriwa katika hospitali ya Mkoa.
  • Mashine ya ultra sound imenunuliwa kwa gharama ya Tsh24,000,000/=, mashine ya kutoa Dawa ya usingizi imenunuliwa kwa gharama ya Tsh 45,000,000/= na Jokofu la kuifadhi damu kwa gharama ya Tsh. 28,000,000/=
  • Wodi tatu kati ya nane sawa na asilimia 37.5 zimefanyiwa ukarabati. Vile vile njia ya kupitisha maiti kwenda mortuary imejengwa. Katika kuboresha utoaji huduma katika hospitali za Halmashauri mambo yafuatayo yamefanyika kwa mwaka 2014/2015;

Katika kuboresha utoaji huduma katika hospitali za Halmashauri  mambo yafuatayo yamefanyika kwa mwaka 2014/2015;

  • Hospitali zote tano za wilaya zimehamasishwa kuanzisha kitengo cha kuhudumia wagonjwa wa dharura (Accident and Emergency department) Hospitali ya shirati na Butiama kati ya hospitali tano wameshaanzisha kitengo hicho sawa na asilimia 40.
  • Hospitali zote tano zina Mashine ya ultra sound ambazo zinasaidia utambuzi wa matatizo ya afya.
  • Hospitali ya Wilaya Tarime iliyokuwa imechakaa sana inafanyiwa ukarabati mkubwa kwa kutumia nguvu za wananchi wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya.

 

Mfuko wa Afya ya Jamii
Mkoa unaendelea kuhamasisha wananchi wajiunge na mfuko wa Afya ya Jamii. Juhudi zinazofanywa kuhakikisha kuwa kazi hii inakuwa na mafanikio ni pamoja na kuhakikisha kuwa Vituo vya kutolea huduma vinakuwa na madawa ya kutosha pamoja na kuongeza uhamasishaji kwa kushirikiana na NHIF. Hadi sasa Kaya zilizojiunga na mfuko wa Afya ya Jamii kati ya asilimia 2 (Tarime TC) na 44.2 (Musoma DC) – Kimkoa ni asilimia 10. Mchanganuo wake unaonekana katika jedwali lifuatalo:


Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Ampokea Meja Jenerali Mani

    May 13, 2025
  • RC azitaka Wilaya kuongeza nguvu maandalizi ya Mwenge 2025

    May 09, 2025
  • Mtambi akabidhi tuzo na kinyago washindi wa Mwenge 2024

    May 09, 2025
  • Mtambi alitaka jukwaa la ushirika kuongeza ubunifu

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa