• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi awasilisha maombi matatu Wizara ya Afya

Posted on: February 18th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 18 Februari, 2026 amempokea Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalage na kuwasilisha maombi matatu kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma za afya katika Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtambi ameiomba Wizara ya Afya kufuatilia kwa karibu ukamilishaji wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inayoendelea kujengwa katika eneo la Kwangwa, Manispaa ya Musoma ili iweze kukamilika kwa haraka na kutoa huduma stahiki za kibingwa na kibobezi kwa wananchi wa Mkoa wa Mara na mikoa jirani.

Mhe. Mtambi ameiomba Wizara ya Afya kufuatilia utendajikazi wa Mshauri Mwelekezi wa Mradi huo ambaye amesema anakwamisha utekelezaji wa mradi na kusababisha fedha zilizotengwa kukamilisha mradi huo kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kutumika kidogo kwa sababu ya kutokutekeleza majukumu yake kama inavyotakiwa.  

“Ukamilishaji wa Hospitali ya hii ulipangiwa shilingi bilioni 10 lakini mpaka wakati huu, mwaka wa fedha ukiwa unakaribia kuisha zimetumika shilingi bilioni 2.1 tu baada ya wakandarasi kuwasilisha madai yao na mshauri mwelekezi kutoyafanyia kazi” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema Mshauri Mwelekezi pia anasababisha wakandarasi waliopo katika mradi huo kushindwa kuendelea kukamilisha mradi wakisubiria idhini ya kuendelea kutoka kwa Mshauri Mwelekezi ili waweze kuendelea kukamilisha mradi na kutekeleza mahitaji mengine yaliyojitokeza katika  mradi huo.

Mhe. Mtambi amesema mradi huo ni moja kati ya miradi ya kimkakati ya Mkoa wa Mara na hivyo kuchelewa kukamilishwa kwa muda mrefu kunaifanya gharama ya mradi huo kuwa kubwa, wananchi kukosa huduma stahiki na kuvuruga mipango ya Serikali katika ukamilishaji wa mradi huo.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mtambi pia ameiomba Wizara ya Afya kuridhia kuwahamisha baadhi ya madaktari wa kawaida wanaofanyakazi Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili wahamishiwe katika Halmashauri za Mkoa wa Mara zenye uhitaji na Madaktari Bingwa waliopo katika baadhi ya Halmashauri za Mkoa wa Mara wahamishiwe Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere ili waweze kutumika vizuri kulingana na utaalamu wao.

Mhe. Mtambi amesema baadhi ya Halmashauri zina madaktari wachache jambo ambalo linaongeza rufaa za wagonjwa ambao wangeweza kutibiwa katika vituo vya afya na Hospitali za Halmashauri lakini kwa kuwa vbaadhi ya vituo hivi havina madaktari inawalazimu kutoa rufaa kwenda Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere.

Aidha, Mhe. Mtambi ameiomba Wizara ya Afya kuwahamishia Madaktari Bingwa wa Upasuaji na Mifupa katika Hospitali za Halmashauri za Wilaya ya Tarime ili kutibu majeruhi wengi wanaojitokeza katika hospitali hizo kwa haraka kabla ya kupelekwa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Musoma au Hospitali ya Rufaa ya Bugando iliyopo Jijini Mwanza kwa matibabu zaidi.

Kanali Mtambi ametumia fursa hiyo kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Mara kuishukuru Wizara ya Afya kwa kuratibu kambi za madaktari bingwa katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na hospitali za Halmashauri na Vituo vya Afya kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Mara.

Kwa upande wake, Dkt. Shekalage ameushukuru Mkoa wa Mara kwa kuchukua hatua mbalimbali katika kufuatilia ukamilishaji wa mradi wa ukamilishaji wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na kumhakikishia kuwa amekuja Mara baada ya kupokea taarifa za mradi huo na anaenda kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

“Nimeambatana na wataalamu wangu tukagua utekelezaji wa mradi na kufanya kikao na wahusika wote katika mradi huo ili kupata hali halisi ya utekelezaji wa mradi kabla ya kufanya maamuzi” amesema Dkt. Shekalage.  

Aidha, Dkt. Shekalage amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kufanya msawazo wa muda wa watumishi wa sekta ya afya waliopo katika Mkoa wa Mara na kuzitaarifu Wizara zinazohusika ili ziweze kuridhia katika na kufuata taratibu za kawaida za Serikali katika kuhamisha watumishi wa umma.

 Mapokezi hayo yamehudhuriwa pia na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Dominicus Lusasi, Maafisa kutoka Wizara ya Afya, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii, Meneja wa NHIF Mkoa wa Mara, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi awasilisha maombi matatu Wizara ya Afya

    February 18, 2026
  • Mtambi azindua kampeni ya utoaji wa dawa kinga

    February 16, 2026
  • Mtambi: Marufuku magari yasiyo na leseni kubeba abiria Mara

    February 13, 2026
  • Mara yajipanga kuboresha ufaulu wa wanafunzi

    February 13, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa