• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mara yajipanga kuboresha ufaulu wa wanafunzi

Posted on: February 13th, 2026

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo tarehe 13 Februari, 2026 amefungua kikao cha majumuisho ya tathmini ya ufaulu kwa mwaka 2025 na kuidhinisha mikakati ya    mwaka 2026 amewataka wasimamizi wa elimu katika Mkoa wa Mara kutimiza wajibu wao katika ufuatiliaji na usimamizi wa ufundishaji ili kuboresha ufaulu wa wanafunzi.

Akizungumza katika ufunguzi wa kikao hicho, Ndugu Kusaya amezitaka Halmashauri zote za Mkoa wa Mara kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuboresha ufaulu kwa mwaka 2026 ili kunyanyua ufaulu wa wanafunzi katika matokeo ya mitihani ya kitaifa.  

“Mkoa wa Mara tunajipanga kufanya mabadiliko makubwa katika sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuongeza mitihani ya majaribio katika ngazi ya shule, kata, Halmashauri na Mkoa ili kuwapima wanafunzi hao na kusahihisha pale tunapoona hatufanyi vizuri kama Mkoa kabla ya mtihani wa kitaifa” amesema Ndugu Kusaya.

Ndugu Kusaya amewatahadharisha kuwa itafika wakati wasimamizi wa elimu kwa ngazi mbalimbali watawajibishwa kulingana na matokeo ya ufaulu wa wanafunzi na kuwataka wasimamizi hao kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuboresha ufaulu wa wanafunzi na hususan shule za msingi na kidato cha kwanza hadi kidato cha nne.

Ndugu Kusaya amewataka wasimamizi wa elimu ngazi ya Mkoa na Halmashauri kufanya maboresho katika usimamizi wa elimu na kuongeza ufuatiliaji wa ufundishaji na ujifunzaji madarasani na kuchukua hatua za haraka ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi.

Ndugu kusaya amesema lengo la kikao hicho ni kuandaa mikakati ya kupandisha ufaulu wa wanafunzi katika Mkoa wa Mara na kuwataka maafisa hao kuitumia vizuri siku hiyo ili kupanga mikakati itakayopandisha ufaulu katika Shule, Kata, Halasmahuri na baadae Mkoa.

Aidha, Ndugu Kusaya amewataka wasimamizi wa Elimu Mkoa wa Mara kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali na hususan wazazi, walezi na viongozi mbalimbali katika jamii ili wasaidie katika kuboresha ufaulu wa wanafunzi.  

Awali akitoa taarifa kwa Katibu Tawala, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Dkt. Elpidius Baganda amesema kikao hicho cha siku moja kina lengo la kufanya majumuisho ya mikakati ya ufaulu iliyopangwa kuanzia ngazi ya shule, Kata na Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mara ili kupata mkakati wa Mkoa wa Mara.

Dkt. Baganda amesema kikao hicho pia kitaandaa ratiba na kuweka mikakati ya matukio yote muhimu ya kielimu kwa mwaka 2026 ikiwemo ufanyikaji wa mitihani ya utayari kwa madarasa yote ya mitihani, mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA na Wiki ya Elimu.

Aidha, Dkt. Baganda amesema kuwa katika kikao hicho pia wasimamizi hao watashirikiana uzoefu katika masuala ya kiutawala na hususani katika usimamizi wa majukumu ya kielimu.

Kwa upande wake, Afisa Elimu wa Sekondari ya Manispaa ya Musoma Ndugu Avith Mallya amemshukuru Katibu Tawala wa Mkoa kwa maelekezo aliyoyatoa ili kuinua ufaulu wa wanafunzi katika Mkoa wa Mara.

“Sisi kama wasimamizi wakuu wa elimu Mkoa wa Mara tunakuahidi tujayafanyia kazi haya maelekezo yote na kuhakikisha tunaboresha kiwango cha taaluma na ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya  ndani nay a Kitaifa” amesema Ndugu Mallya.

Aidha, Ndugu Mallya ameahidi kuwa kama wasimamizi wa Elimu watatekeleza mikakati yote itakayopangwa katika kikao hicho kwa kushirikiana na wadau wa elimu kwa lengo la kuboresha ufaulu wa wanafunzi.

 Kikao hicho kimehudhuriwa na baadhi ya Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Maafisa Elimu Msingi, Sekondari, Taaluma, Takwimu na Vifaa, Elimu Maalum, Wadhibiti Ubora na Maafisa wa TSC kutoka Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mara na kimefanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Ufundi Musoma.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi: Marufuku magari yasiyo na leseni kubeba abiria Mara

    February 13, 2026
  • Mara yajipanga kuboresha ufaulu wa wanafunzi

    February 13, 2026
  • BILIONI 38 kuwasha umeme vitongoji 371 Mara

    February 12, 2026
  • RC Mtambi kuwaongoza watumishi mazishi ya Saaban Ndalu

    January 30, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa