• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi azindua kampeni ya utoaji wa dawa kinga

Posted on: February 16th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 16 Februari, 2026 amezindua kampeni ya utoaji wa dawa kinga dhidi ya minyoo, tumbo na kichocho katika Shule ya Msingi Mazoezi, iliyopo Chuo cha Ualimu Bunda na kuwataka wananchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kuanzia miaka minne wanapata dawa kinga hizo ili kujilinda dhidi ya magonjwa.

“Kama Mkoa tunachukua hatua zote kutokomeza magonjwa yasiyopewa kipaumbele na mtu yoyote anaposikia dalili za magonjwa hayo afike hospitali mapema” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi ameyataja magonjwa yanayohusika na kampeni hiyo kuwa ni pamoja na matende, mabusha, usubi, kichocho na minyoo na kueleza kuwa katika Mkoa wa Mara magonjwa yanayosumbua zaidi kati ya hayo ni kichocho na minyoo.

Aidha, Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuelezea kuhusu kampeni nyingine za sekta ya afya ikiwemo utoaji wa bima ya afya kwa wote na kampeni ya kutokomeza vifo vya akina mama wajawazito wakati na baada ya kujifungua na watoto wachanga.

Akizungumzia kuhusu bima ya afya kwa wote, Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara umeshaanza kutoa kadi za matibabu kwa makundi maalum yaliyolipiwa na Serikali ikiwemo wananchi wanaotoka kaya maskini na wazee wasiojiweza.

Mhe. Mtambi amewahamasisha wananchi wote wa Mkoa wa Mara kujiunga na mpango wa bima ya afya kwa wote ili waweze kunufaika na huduma za afya na kupata uhakika wa matibabu katika hali yofauti za kiuchumi pindi matatizo yanapowafika.

Kanali Mtambi amesema Mkoa unaendelea kuboresha huduma za afya kwa kujenga vituo vipya vya kutolea huduma za afya, magari ya kubebea wagonjwa ambapo kupitia Mpango wa MMAMA Serikali imeweka utaratibu wa usafiri wa bure kwa wajawazito na watoto wachanga.

Mhe. Mtambi amewahamasisha akina mama wajawazito kuanza na kuhudhuria kliniki ili waweze kupata huduma za vipimo na ushauri wa kitaalamu kuhusiana na namna ya kuulea ujauzito kutokana na hali zao za kiafya na hatimaye kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma za afya walivyoshauriwa.

Awali, akizungumza wakati wa Kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Aswege Enock Kaminyonge alisema kuwa hali ya wanafunzi kuripoti shuleni katika Wilaya ya Bunda ni nzuri kwa kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi waliotakiwa kuanza shule za awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza wameripoti na wanaendelea na masomo.  

Akitoa taarifa ya zoezi hilo, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt. Zabron Masatu amesema zoezi hilo litakalofanyika kwa siku tatu linategemea kutoa dawa kinga kwa watoto zaidi ya laki sita wa Mkoa wa Mara wenye umri wa miaka 4 hadi 14.

Dkt. Masatu amesema zoezi hilo litahusisha zaidi wanafunzi waliopo shule na kuwashukuru walimu kwa ushirikiano wao katika kuhakikisha watoto wote wanapata dawa kinga hizo ili kuwalinda kutokana na magonjwa hayo.

Kampeni hiyo inayofanyika kwa siku tatu katika Mkoa wa Mara inaongozwa na Kauli Mbiu “Tuungane, Tuchukue hatua, Kutokomeza Magonjwa yaliyokuwa hayapewi kipaumbele”. 

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi azindua kampeni ya utoaji wa dawa kinga

    February 16, 2026
  • Mtambi: Marufuku magari yasiyo na leseni kubeba abiria Mara

    February 13, 2026
  • Mara yajipanga kuboresha ufaulu wa wanafunzi

    February 13, 2026
  • BILIONI 38 kuwasha umeme vitongoji 371 Mara

    February 12, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa