• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi: Marufuku magari yasiyo na leseni kubeba abiria Mara

Posted on: February 13th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo amefanya kikao cha wadau wa usafirishaji wa Mkoa wa Mara katika ukumbi wa uwekezaji na kupiga marufuku magari yasiyo na leseni za kusafirisha abiria kubeba abiria katika Mkoa wa Mara.

Akizungumza katika kikao hicho Mhe. Mtambi amewataka wafanyabiashara wa sekta ya usafirishaji kufuata taratibu, kanuni na sheria za usafirishaji wakati wote wanapotoa huduma za usafirishaji kwa wananchi na kutoa huduma bora kwa wasafiri na kuboresha huduma zao wakati wote wanapohitajika kufanya hivyo.

“Vyombo vya usalama simamieni sheria, taratibu na kanuni ili wafanyabiashara hawa wafanye biashara zao kwa mujibu wa matakwa ya leseni zao na kuhakikisha abiria wanapata huduma bora ya usafiri wakati wote” amesema Mhe. Mtambi.  

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara ameunda timu ndogo ya kupitia kwa undani na kutoa mapendekezo ya mgogoro wa mabasi madogo ya abiria na magari madogo abiria aina ya probox na succed katika kituo cha magari Buhemba, Wilaya ya Butiama na kuitaka kufanyakazi kwa siku 21 kuanzia Jumatatu tarehe 16 Februari, 2026 na kuwasilisha mapendekezo ofisini kwake ya namna ya kutatua mgogoro huo.  

Mhe. Mtambi amemteua Mwenyekiti wa Wajasiriamali Mkoa wa Mara kuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Katibu wa Wasafirishaji wa Mkoa wa Mara kuwa Katibu wa Kamati hiyo, Mwenyeviti wa Madereva wa Bajaji na Bodaboda na wajumbe wawili wamiliki wa gari aina ya succeed/probox wanaofanya shughuli zao katika kituo hicho.

Wajumbe wengine walioteuliwa ni Ndugu Joseph Cosmas na Frank Peter ambao ni wamiliki wa mabasi madogo kuwa wajumbe wa kamati hiyo wakati Ndugu George Robert Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Mara, Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani SP Adribert Ntilicha kuwa washauri katika kamati hiyo.

Mhe. Mtambi amesema wakati timu aliyoiunda ikiendelea kutekeleza jukumu lake, huduma za usafirishaji katika eneo la Buhemba ziendelee kama zilivyokuwa hapo awali, mabadiliko yatafanyika baada ya timu iliyoundwa kukamilisha jukumu lake na kutoa mapendekezo.  

Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuwapongeza madereva wa pikipiki na bajaji Mkoa wa Mara kwa mabadiliko makubwa wanayoyaonyesha baada ya kushiriki mafunzo ya udereva yaliyoendeshwa na Mamlaka ya Ufundi (VETA) Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa madereva hao kuendelea kuwahamasisha madereva wote kupata mafunzo na leseni na kuboresha uendeshaji wao ili kutoa huduma bora kwa wananchi na kuwaahidi kuwatafutia wadau watakaowanunulia unifomu ili waendelee kuwa nadhifu wakati wote wanapotoa huduma.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Wasafirishaji Mkoa wa Mara Ndugu Sibogo Julius Mhoni amesema kuwa tangu kikao cha mwisho kilichofanyika Oktoba, 2025, mambo mengi yametekelezwa lakini bado kuna changamoto bado hazijatatuliwa.

Ndugu Mhoni amezitaja changamoto ambazo bado hazijatatuliwa kuwa ni pamoja na magari yasiyo na leseni kusafirisha abiria na mizigo magari yamekuwa mengi na mabasi ya abiria yanakuwa hayapati abiria kutokana na uwingi wa magari hayo.  

“Changamoto nyingine ambazo bado zinajitokeza ni pamoja na polisi kuendelea kuwanyang’anya madereva leseni zao, n ahata leo kuna baadhi ya madereva wamenyang’anywa leseni” amesema Ndugu Mhoni.  

Kwa upande wake, Ndugu George Robert Afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Mara amesema katika kituo cha Buhemba, magari aina ya probox /Succeed ambayo yana lesseni hayazidi matatu, kuna magari mengine yaliyopo hayana leseni za usafirishaji wa abiria.

Ndugu Robert amesema magari yote yanalipia fedha kulingana na uwezo wa gari na kwa hiyo gari aina ya probox yenye lesseni yanalipia shilingi 35,000 wakati basi ndogo za abiria zinalipia 45,000 kwa mwaka.

Ndugu Robert amesema LATRA huwa inayakamata magari ambayo hayana leseni za usafirishaji wa abiria lakini kwa mujibu wa leseni za magari madogo abiria wanapatana na wamiliki kuhusu nauli na Serikali haiingilii makubaliano yao.

 Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Kamati ya Usalama ya Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Mwenyekiti wa Wajasiliamali Mkoa wa Mara, baadhi ya wakuu wa taasisi za Serikali, Makamanda wa Vikosi vya Usalama Barabarani.   

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi: Marufuku magari yasiyo na leseni kubeba abiria Mara

    February 13, 2026
  • Mara yajipanga kuboresha ufaulu wa wanafunzi

    February 13, 2026
  • BILIONI 38 kuwasha umeme vitongoji 371 Mara

    February 12, 2026
  • RC Mtambi kuwaongoza watumishi mazishi ya Saaban Ndalu

    January 30, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa