• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi alipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mara

Posted on: October 27th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 26 Oktoba, 2025 amezindua magari manne ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara na amelipongeza Jeshi hilo kwa kazi nzuri wanayoifanya katika Mkoa wa Mara.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua magari hayo, Mhe. Mtambi amesema Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya kazi nzuri katika Mkoa wa Mara na hususan uokoaji katika ajali mbalimbali zinazotokea nchi kavu na katika maji.

“Mimi ninawaomba muendelee kufanyakazi kwa weledi na mboreshe zaidi utendaji wenu baada ya kupokea vifaa na magari haya ili wananchi wa Mkoa wa Mara wapate huduma nzuri” amesema Mhe. Mtambi.

Akitoa ufafanuzi wa utendaji wa Jeshi hilo, Mhe. Mtambi amesema jeshi hilo linatumia muda mfupi baada ya kupata taarifa ya majanga au ajali kufika katika eneo husika na kuanza kufanya kazi ya uokoaji.

Kanali Mtambi kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Mara ameishukuru Serikali kwa kutoa magari na vifaa vya uokoaji ambavyo amesema ni muhimu sana katika kukabiliana na majanga ya uokoaji na kulitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuyatumia magari hayo kwa shughuli zilizokusudiwa.

Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo pia kuwahamasisha wananchi wa Mkoa wa Mara kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapa nchini tarehe 29 Oktoba, 2025 na kuwataka kuondoa hofu kwa kuwa Serikali ya Mkoa wa Mara imejiandaa kulinda amani na utulivu wakati na baada ya uchaguzi.

Wakati huo huo, Mhe. Mtambi amewataka wananchi kujenga baada ya kupata vibali vya ujenzi ili kuepuka ujenzi holela, amewaagiza watendaji wa Serikali kuhakikisha majengo yote ya Serikali yanafuata kanuni za usalama na wananchi walitumie jeshi hilo kupata ushauri wa kiutalaamu.

Aidha, Mhe. Mtambi amewakemea wananchi wanaoharibu miundombinu ya zimamoto na kupiga namba za dharura na kutoa taarifa za uongo na kulitaka jeshi hilo kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.

Kwa upande wake, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara Agustine Boniphace Magere amesema Mkoa wa Mara umepokea magari mapya manne kwa sasa na wanategemea magari mengine matatu kwa siku za hivi karibuni.

“Magari ambayo tumeyapokea ni pamoja na gari la kuzima moto, gari la kubeba wagonjwa, gari ya utangulizi na gari ya ukaguzi” amesema Kamanda Magere na kuongeza kuwa anategemea magari hayo yataimarisha utendaji kazi wa jeshi hilo katika Mkoa wa Mara.

Awali akitoa taarifa ya Jehi hilo, Kamanda Magere amesema kwa sasa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara lina vituo sita vya zimamoto katika Mkoa wa Mara na kwa kipindi cha Julai hadi Septemba, 2025 Mkoa umepata matukio ya ajali tisa.

Kamanda Magere ameyataja mafanikio yaliyopatikana katika Jeshi hilo Mkoa wa Mara ni pamoja na kufanikiwa kupata viwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za jeshi hilo ambapo wanategemea ujenzi utaanza katika mwaka wa fedha 2025/2026 na mafanikio mengine ni vitendea kazi na magari waliyoyapata ambayo amesema vitaongeza ari ya utendaji kazi na kuboresha huduma kwa wananchi.

Kamanda Magere amezitaja changamoto za Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara kuwa ni pamoja na ujenzi holela wa makazi, wananchi kupiga namba ya dharura 114 na kutoa taarifa za uongo, wananchi kuharibu miundombunu ya zimamoto.

Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa amekagua pia magari yaliyopokelewa pamoja na kupata taarifa za magari hayo na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara.

Uzinduzi wa magari hayo umehudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara, Mkurugenzi na Menejimenti ya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, Wakuu wa Taasisi za umma, maaskari na watumishi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Mara aunda Kamati kuchunguza ratiba za mabasi madogo

    October 27, 2025
  • Mtambi alipongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mara

    October 27, 2025
  • Wananchi Mara wahimizwa kupiga kura kwa amani na utulivu

    October 25, 2025
  • Mtambi awataka wakulima Bunda na Musoma kuchangamkia fursa ya kilimo cha choroko

    October 24, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa