• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC Mara ateta na Viongozi wa Dini

Posted on: January 13th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 13 Januari, 2026 amezungumza na viongozi wa Kamati ya Amani na Maridhiano na kuwaomba Viongozi wa Dini kuisaidia Serikali katika kampeni ya kutokomeza ukeketaji na kudhibiti vifo vinavyotokana na uzazi kwa wanawake wajawazito.

Akizungumza kuhusu ukeketaji, Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara kupitia Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) imeazimia kutumia njia mbalimbali na makundi mbalimbali ya watu kutoa elimu kwa wananchi ili kudhibiti masuala hayo.

“Ninyi Viongozi wa Dini mtusaidie kuwaihamasisha wananchi kupitia kwa waumini wa dini mbalimbali kuhusiana na ukeketaji na madhara yake kwa wanawake waliokeketwa” amesema Mhe. Mtambi na kuongeza kuwa wadau wote wakiungana, ukeketaji unaweza kutokomezwa katika jamii.

Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara pia kupitia RCC umeazimia kuwa katika Wilaya zenye ukeketaji, ajenda ya ukeketaji iwe ni ajenda ya kuduma katika vikao na mikutano yote inayofanyika ili kutoa elimu ya mara kwa mara kwa makundi mbalimbali.   

Akizungumza kuhusiana na vifo vya wanawake wakati wa kujifungua, Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara unapata vifo vya wanawake wakati wa kujifungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo wanawake wajawazito kutokuhudhuria kliniki na kutokufuata maelekezo ya wataalamu wa afya.

Mhe. Mtambi amesema Serikali imeboresha sana upatikanaji wa huduma za afya kwa kuhakikisha wataalamu, miundombinu na vifaa tiba vipo katika vituo vya kutolea huduma za afya lakini wanawake wajawazito hawahudhulii kliniki na wachache wanaohudhuria hawatekelezi maelekezo ya wataalamu wa afya.

Mhe. Mtambi amewataka Viongozi wa Dini kuwahamasisha waumini kuhudhuria kliniki, kupima afya zao na kufuata ushauri wa wataalamu wa afya kuhusu vyakula, kutumia dawa za kuongeza damu, kuwahi hospitali wakipata uchungu na ushauri mwingine wanaopewa na wataalamu hao.

Katika kikao hicho Mhe. Mtambi pia amewapokea viongozi wa Redio Tetemo FM walioambatana na Viongozi wa Dini kwa lengo la kutambulisha Redio hiyo yenye ofisi zake katika Manispaa ya Musoma na kuomba Mkuu wa Mkoa wa Mara awe mlezi wa redio hiyo yenye leseni ya kurusha matangazo yake katika Mkoa wa Mara.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Redio Tetemo FM Ndugu Francis Mukirya amesema kuwa redio hiyo wamiliki wake ni pamoja na Askofu Mkuu wa Kanisa la New Life Gospel Community Church maarufu kama Kanisa la Bonde la Baraka, Ndugu Daniel Ouma, ameahidi kusaidia Mkoa wa Mara katika kuhamasisha jamii katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo suala la ukeketaji na vifo vya wajawazito wakati wa kujifungua.

Ndugu Mukirya amesema redio hiyo yenye kauli mbiu yake Habarika, Hamasika inamuomba Mkuu wa Mkoa awe mlezi wake pamoja na kuishauri, kuitambulisha redio hiyo kwa taasisi za Serikali na wadau na kuishirikisha katika matukio mbalimbali ya Mkoa.  

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SIMAUJATA) Mkoa wa Mara Ndugu Joyce James aliambatana na viongozi wa dini amewaomba viongozi wa dini kuwahamasisha waumini kuhusiana na suala la malezi na makuzi ya watoto ili kujenga jamii yenye maadili mema na kumwogopa Mungu.

Ndugu Joyce amesema wazazi wengi wanatoa matunzo ya watoto lakini kwenye malezi hawatoi mifano mizuri wala elimu kuhusu watoto hao wanavyopaswa kuishi katika jamii na mara nyingi hawaendi nao katika nyumba za ibada jambo ambalo linaonyesha kuwa watoto hawapati mafundisho ya dini kama inavyotakiwa.

Mkuu wa Mkoa kukutana na viongozi wa dini ni sehemu ya utaratibu wake wa kawaida aliojiwekea wa kukutana na viongozi wa dini mara kwa mara ili kuwashirikisha katika mipango, mikakati ya Mkoa wa Mara kuhusiana na masuala mbalimbali.  

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Mara ateta na Viongozi wa Dini

    January 13, 2026
  • Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi yaingia Mara

    January 08, 2026
  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa