• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi yaingia Mara

Posted on: January 8th, 2026

Wajumbe wa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amania yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu tarehe 29 Oktoba, 2025 leo wamewasili Mkoa wa Mara wakiongozwa na Balozi Radhia Msuya na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi.  

Akizungumza wakati wa mapokezi, Balozi Msuya amesema wao ni sehemu ya Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi Mkuu, 2025 na siku zilizofuata ambapo ilitokea kadhia iliyopolekea watu kupoteza maisha, kuumia, mali kuteketea, kwa hiyo Mhe. Rais ameunda tume ili kuchunguza kitu gani kimetokea, madhara gani yamepatikana na nini kifanyike.  

“Tanzania hatukuwa na kawaida ya yale tuliyoyaona tarehe 29 Oktoba, 2025, tumefikaje na tutatokaje hapa” amesema Balozi Radhia na kuongeza kuwa Tume hiyo ina makamishana tisa na inaongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu Mohammed Chande Othman na imepewa siku 90 za kufanyakazi hiyo.  

Balozi Msuya amesema kwa sasa tayari wamefanya kazi Mkoa wa Dar es Salaam na kwa sasa wapo mikoani na tayari wajumbe wamegawanyika makundi matatu wengine wameenda mikoa ya Kilimanjaro na Arusha; Mbeya na Songwe na wengine wapo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa wajumbe wa Tume walianzia Mkoa wa Mwanza kwa siku nne na baadaye kugawanyika vikundi viwili ambapo baadhi wameenda Geita na wengine wapo Mkoa wa Mara ambapo wanatarajia kufanya kazi kwa siku tatu kuanzia leo tarehe 08-10 Januari, 2026.

Balozi Msuya amepongeza maendeleo mbalimbali yaliyopatikana katika Mkoa wa Mara tangu mara ya mwisho alipotembelea na kuongeza kuwa anaamini Tanzania itasonga mbele kiuchumi na kijamii kutokana na nyenzo mbalimbali zilizopo.

Kwa upande wake, Balozi David Kapya amesema Tume hiyo itaangalia hali ilikuwaje wakati wa matukio hayo, ilidhibitiwa kwa namna gani pamoja na kusikiliza maoni, malalamiko, ushauri kutoka kwa uongozi na timu ya Mkoa na wananchi.

Akizungumza katika Mapokezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Mtambi amewakaribisha wajumbe wa kamati hiyo na kuwahakikishia kuwa Mkoa wa Mara upo salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kawaida.

Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara una matumaini makubwa na Tume ya uchunguzi katika kutoa mapendekezo yenye tija yatakayoitoa nchi sehemu ilipofikia kwa sasa hivi ili kulisaidia Taifa kudumisha amani na mshikamano wa kitaifa wakati wote. 

Baada ya kupokelewa tume hiyo itafanya mahojiano na Kamati ya Usalama ya Mkoa, maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara na Mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya na Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii na wasimamizi na maafisa mbalimbali wa sekta ya afya Mkoa wa Mara.

Tarehe 09 Januari, 2026 Tume itafanya mahojiano na makundi maalum ya vijana, kutembelea magereza, mahojiano na Kamati ya Usalama ya Wilaya wakati tarehe 10 Tume itafanya mahojiano na Kamati ya Usalama ya Wilaya na mahojiano na wananchi walioathirika na makundi maalum.

Mapokezi hayo pia yalihudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara na Maafisa walioambatana na wajumbe wa tume hiyo na Maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara. 

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi yaingia Mara

    January 08, 2026
  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa