• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

Posted on: January 6th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 06 Januari, 2025 ameongoza kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mara (RCC) na kueleza kuwa Mkoa wa Mara haitamvumilia mtu yoyote atakayeiyumbisha sekta ya elimu.

Mhe. Mtambi amesema hayo wakati wa kujadili taarifa ya maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza katika mwaka wa masomo 2026 ambapo ameitaka Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwasilisha kuwasilisha taarifa ya maandalizi ya mapokezi ya wanafunzi wa awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza kwa mwaka 2026 siku ya Ijumaa tarehe 09 Januari, 2026 saa 2 kamili asubuhi.  

“Ninataka iwasilishwe pia taarifa ya sababu za ufaulu mbovu wa wanafunzi katika Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka 2025 ambapo matokeo ya mtihani yanaonyesha kuwa Mkoa wa Mara ulikuwa wa mwisho na ninahitaji sababu za kitaalamu za matokeo hayo” amesema Mtambi.

Mhe. Mtambi amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kuhakikisha kuwa taarifa hiyo itakapowasilishwa Wakuu wa Sehemu na Vitengo vya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara wawepo na kuwataka wasimamizi wote wa sekta ya elimu wakiwemo Maafisa Elimu Kata, Wakaguzi wa Shule na Wadhibiti Ubora kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Ninataka kila mtu atomize wajibu wake na wajitahidi kutatua changamoto katika maeneo yao, kama walimu hawatoshi wao wanaweza kuingia madarasani na kufundisha kwa sababu wao ni walimu na kazi ya kusimamia hawaifanyi wakati wote” amesema Mhe. Mtambi.

Kanali Mtambi amesema kwa historia Mkoa wa Mara umekuwa ukifanya vizuri katika elimu na kukumbushia Azimio la Musoma la Mwaka 1974 ambalo lilisistiza umuhimu wa elimu kwa maendeleo endelevu ya Taifa ambalo liliasisiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na likaleta matokeo chanya katika maendeleo ya elimu hapa nchini.

Mhe. Mtambi amesistiza msimamo wa Mkoa wa Mara kuhakikisha wanafunzi wote wanapatiwa chakula shuleni na kuwataka Wakuu wa Wilaya, wasimamizi wa sekta ya elimu na viongozi wote wa Mkoa Mara kuhakikisha shule zote zinatoa chakula shuleni na wanafunzi wote wanaotakiwa kuanza shule wanaenda shule zitakapofunguliwa.

“Kama wanafunzi hawapelekwi shule, viongozi tuchukue hatua, watoto wasome, kuna sheria za nchi a sheria ndogondogo tuzitumie kuhakikisha watoto wote wanaotakiwa kuanza shule wanaanza” amesema Mhe. Mtambi.

Kanali Mtambi amewataka wazazi na walezi wa wanafunzi kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi na hususan kuwapeleka watoto shule, kuhakikisha wanapata angalau mlo mmoja wakiwa shule na wanaishi katika mazingira salama nyumbani na katika jamii.

Mhe. Mtambi amesema elimu ni suala muhimu sana katika ustawi na maendeleo ya jamii na haliwezi kuachiwa likafanyika kiholela bila kusimamiwa kwa ukaribu na kutoa onyo kwa watumishi wote wa sekta ya elimu kujitathmini na kukemea uzembe na kutokuwajibika katika kutekeleza majukumu yao.

Taarifa nyingine zilizopokelewa na kujadiliwa katika kikao cha RCC ni pamoja na taarifa ya mwenendo wa uzalishaji mali katika Mkoa wa Mara; taarifa ya utekelezaji wa Mpangokazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto Awamu ya Pili; taarifa ya maendeleo ya sekta ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoa wa Mara.

Taarifa nyingine zilizopokelewa na kujadiliwa katika kikao hicho ni taarifa ya upatikanaji wa maji Mkoa wa Mara; na taarifa ya upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Mara.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Mkoa, wabunge, Meya, Wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara, Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa, maafisa kutoka taasisi za umma, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wadau wa maendeleo na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya kiraia.  

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Mara yaazimia kufuatilia utekelezaji wa miradi ya barabara

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa