• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC Mtambi kuwaongoza watumishi mazishi ya Saaban Ndalu

Posted on: January 30th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi anatarajiwa kuwaongoza watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mara katika mazishi ya Mhasibu Mkuu Daraja la 1 CPA. Shaaban Chissebe Ndalu aliyefariki leo tarehe 30 Januari, 2026 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma anayetarajiwa kuzikwa Jumatatu tarehe 02 Februari, 2026 nyumbani kwake katika eneo la Mpuguzi, Dodoma.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa za msiba huo, Mhe. Mtambi ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu kwa msiba huo na amesema kuwa pengo aliloliacha halitaweza kuzibika kiurahisi na marehemu atakumbukwa kwa uhodari na uchapakazi wake.  

Katika safari hiyo, Mhe. Mtambi ataambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya na maafisa wengine wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mara ili kushiriki mazishi hayo.

Marehemu Ndalu alizaliwa tarehe 11 Julai, 1975 Chibelela, katika Wilaya ya Bahi, Mkoa wa Dodoma na alihitimu darasa la saba Shule ya Msingi Chibelela mwaka 1990 na akafaulu kwenda Shule ya Sekondari ya Azania, Dar es Salaam ambapo alihitimu mwaka 1994 na alichaguliwa kwenda Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari ya Mazengo, Dodoma ambapo alihitimu mwaka 1997.

Ndugu Ndalu alihitimu Diploma ya Juu ya Uhasibu kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) mwaka 2004, Diploma ya Uzamili katika Uhasibu kutoka Chuo cha Uhasibu Arusha mwaka 2006 na baadaye alipata Cheti cha Uhasibu wa Umma (CPA) mwaka 2017.

Ndugu Ndalu aliajiriwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mwaka 2005 kama Mhasibu wa miradi na baadae akapandishwa vyeo hadi Disemba, 2027 alipoteuliwa kuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara hadi mwaka 2018 alipohamishiwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kama Kaimu Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara.

Mwaka 2020 Ndalu alithibitishwa kama Mkuu wa Idara ya Fedha na Biashara katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na alifanya kazi hadi Julai, 2022 alipohamishiwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kama Mhasibu Mkuu Daraja la 1 hadi leo tarehe 30 Januari, 2026 alipofariki.   

Marehemu Ndalu amefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi na kulazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Dodoma wakati akiwa katika likizo yake ya mwaka na baada ya matibabu alipata nafuu na kutolewa hospitali hata hivyo hali yake ilibadilika tarehe 28 Januari, 2026 ambapo alirudishwa hospitali na akalazwa hadi mauti yalipomkuta.

Marehemu Ndalu ameacha mke na watoto watatu.

Bwana ametoa, Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe!

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC Mtambi kuwaongoza watumishi mazishi ya Saaban Ndalu

    January 30, 2026
  • TISEZA yazindua dawati la uwekezaji Mara

    January 27, 2026
  • TISEZA yahamasisha uwekezaji katika fursa za Mkoa wa Mara

    January 24, 2026
  • Mtambi afanya ziara Butiama

    January 20, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa