• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi awataka wakandarasi Mara kutekeleza miradi usiku na mchana

Posted on: November 8th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 08 Novemba, 2025 amekagua barabara ya Makutano- Nyamuswa- Ikoma Gate sehemu ya Sanzate – Natta na kurudia maelekezo yake ya kuwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya maendeleo katika Mkoa wa Mara kufanyakazi usiku na mchana.  

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo, Mhe. Mtambi amewataka wakandarasi na wazabuni wanaotekeleza miradi mbalimbali katika Mkoa wa Mara kufanyakazi kwa bidi ili kukamilisha kwa haraka miradi ya huduma za jamii kama vile hospitali, shule, barabara na kadhalika.

“Shughuli za ukaguzi wa miradi kwa sasa ndio zimeanza, niwaombe wakandarasi na wazabuni mliopewa kazi ndani ya Mkoa wa Mara kuhakikisha mnafanyakazi usiku na mchana ili kukamilisha miradi mliyopewa kwa wakati ili kuwawezesha wananchi kupata huduma stahiki” amesema Mhe. Mtambi.

Kanali Mtambi amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuweka jitihada thabiti ili kuhakikisha Mkoa wa Mara unatekeleza miradi ya kimkakati ambayo itakuwa chachu ya kurahisisha shughuli mbalimbali za uchumi na kijamii kwa wananchi na kuwataka wakandarasi kutimiza majukumu yao ili malengo ya Serikali yaweze kutimia.

Mhe. Mtambi ametoa rai kwa vyombo vya usalama katika Mkoa wa Mara kusimamia kwa weredi ulinzi wa miradi ya maendeleo inayotekelelezwa pamoja na kuwahamasisha wananchi kudumisha amani na utulivu katika maeneo yao.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi wa Mkoa wa Mara kutowalinda na kuwahifadhi wahalifu na wanaochochea vurugu hapa nchini na kuwaasa kuwa kwa kufanya hivyo wanakuwa ni sehemu ya wanaoharibu amani na utulivu katika jamii.

“Ukimuona mtu ambaye anafanya vitendo vya kuharibu miundombinu ya Serikali, taasisi au watu binafsi mwakemee na ikishindikana mtoe taarifa kwa Jeshi la Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa na msikubali kuwalinda na kuwahifadhi wahalifu” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewahakikishia wananchi kuwa Mkoa wa Mara upo salama na kuwataka watumishi, wananchi, wanafunzi kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kujiletea maendeleo wakati vyombo vya usalama vikiendelea kulinda amani na usalama.   

Aidha, Mhe. Mtambi amewataka wananchi kuitunza miradi inayotekelezwa katika maeneo yao kwa kuwa wao ni wanufaika wa miradi hiyo pamoja na kufanyakazi kwa bidii, kuacha kukochea au kujihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani ikiwemo uharibifu wa miundombinu.

Akizungumzia kuhusu mradi huo, Mhe. Mtambi ameitaka TANROADS kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mradi huo ili kuhakikisha unatekelezwa kwa viwango vya ubora na kwa wakati na hakikisha barabara hiyo inakamilika katika muda uliopangwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Angelina Marco amesema Wilaya ya Serengeti ipo salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao ikiwemo wanafunzi kuendelea na masomo yao kama kawaida.

“Kwa sasa Wilaya ya Serengeti ipo salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za kawaida” amesema Mhe. Marco.

Mhe. Marco amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kutembelea na kuukagua mradi huo ambao amesema umekwama kwa muda mrefu na wananchi wanahamu ya kuuona unakamilika na barabara hiyo ikitumika.   

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe amesema barabara ya Sanzate –Natta ni sehemu ya Barabara ya kutoka Musoma kuelekea Arusha kupitia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Ngorongoro na Mto wa Mbu.  

Mhandisi Maribe amesema mradi huo unatekelezwa na China Railway Seventh Group Co. LTD (CRSG) kutoka nchini China na mkataba wa ujenzi wa mradi huo ulitiwa saini tarehe 02 Aprili, 2020 na ulitakiwa kutekelezwa kwa muda wa miezi 24 kwa gharama ya shilingi milioni bilioni 52.7.

“Kwa sasa Mkandarasi anaendelea kuteleza mradi huu hadi tarehe 20 Januari, 2026 na tayari ameshaomba kuongezewa muda wa mwaka mmoja ili aweze kukamilisha mkataba huu” amesema Mhandisi Maribe.  

Mhandisi Maribe amesema kuwa mradi upo katika asilimia 56 ya utekelezaji wake na tayari mkandarasi ameshalipwa zaidi ya shilingi bilioni 10.4 na bado mkandarasi anadai shilingi bilioni 3.7 na kufafanua kuwa changamoto kubwa katika utekelezaji wa mradi huo ni kuchelewa kwa malipo ya mkandarasi wa mradi huo.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa ameambatana na Kamati ya Usalam ya Mkoa na Wilaya ya Serengeti, viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, maafisa kutoka TANROADS na wakandarasi wa mradi huo.  

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi awataka wakandarasi Mara kutekeleza miradi usiku na mchana

    November 08, 2025
  • Mtambi: Jitokezeni kupiga kura

    October 29, 2025
  • RC Mtambi: Mara ni salama, twendeni tukapige kura

    October 28, 2025
  • RC Mara aunda Kamati kuchunguza ratiba za mabasi madogo

    October 27, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa