• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kusaya: wataalamu wa kilimo fanikisheni Mpango wa Mageuzi ya Kilimo 2050

Posted on: October 24th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo amefungua warsha ya kuwajengea uwezo wataalam kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Halmashauri za Mkoa wa Mara na kuwataka wataalamu wa kilimo kutekeleza kwa ufanisi mpango wa mageuzi ya kilimo 2050.

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha hiyo, Ndugu Kusaya amewataka wataalamu hao kuondoa dhana iliyojengeka katika jamii kuwa kilimo ni adhabu kwa kuwaonyesha fursa mbalimbali zinazoletwa na mpango huu wa mageuzi ya kilimo hapa nchini ili waweze kuzichangamkia na kuinua hali yao ya uchumi.

“Mnao wajibu wa kukiondoa kilimo katika hali ya sasa na kukifanya kuwa miungoni mwa sekta muhimu hapa nchini ambayo ikitumika vizuri itamkomboa mkulima kuondokana na umaskini na kukuza uchumi wa familia hadi Taifa” amesema Ndugu Kusaya.

Kusaya amebainisha kuwa wataalamu wa sekta ya kilimo wakitimiza wajibu wao katika kusimamia kilimo na kuziunganisha sekta za uvuvi, ufugaji na kilimo ili kuongeza tija na kuimarisha uchumi jumuishi katika jamii.

Ndugu Kusaya amewataka wataalamu wa kilimo kusimamia mabadiliko katika sekta ya kilimo ili yaonekane na kuachana na kilimo cha mazoea kinachofanywa na wakulima na kuchukuliwa kama ni kazi ya watu maskini katika jamii, wakati kilimo kikifanyika vizuri kinauwezo wa kuzalisha matajiri wengi sana kiurahisi.

Ndugu Kusaya amesema mpango huo unalenga kuinua hali ya uchumi ya wakulima wa kawaida na hususan waliopo katika maeneo ya vijijini ambao wanaweza kuachana na kilimo cha kujikimu na kufanya kilimo cha biashara na kuuza mazao yao katika soko la dunia.

Kwa upande wake, Mkurugenzi kutoka Ofisi ya Mageuzi ya Kilimo (OTA) Ndugu Elizabeth Misokia amesema Serikali imeanzisha mpango wa mageuzi ya kilimo 2050 kutokana na umuhimu wa sekta ya kilimo katika kufanikisha malengo ya dira ya Taifa ya 2025/2050.

Ndugu Misokia amesema utekelezaji wa mpango huo utasaidia kuleta mageuzi ya kilimo na kuifanya kuwa sekta yenye tija kwa wakulima na mchango mkubwa kwa ukuaji wa pato la mtu mmoja mmoja na pato la Taifa kwa ujumla.

Amesema mpango huo unahusisha kilimo cha mazao 20 ambayo yatatumika kwa ajili ya kuleta mageuzi ya kilimo na usalama wa chakula na kilimo biashara kwa ajili ya masoko ya ndani na nje ya nchi.

Ndugu Misokia ameyataja mazao yaliyopewa kipaumbele katika mpango huu ni pamoja na mazao ya bustani, ngano, pamba, matunda, maziwa, kunde, korosho, kahawa, viungo, ufugaji wa samaki, malisho ya mifugo, kuku, alizeti, katani, mpunga, mahindi, nyama na soya.

Warsha hiyo imehudhuriwa na wataalamu wa kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mara na maafisa kutoka OTA.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi awataka wakulima Bunda na Musoma kuchangamkia fursa ya kilimo cha choroko

    October 24, 2025
  • Kusaya: wataalamu wa kilimo fanikisheni Mpango wa Mageuzi ya Kilimo 2050

    October 24, 2025
  • Demokrasia inaendelea kupevuka katika Mkoa wa Mara: Mtambi

    October 16, 2025
  • Biteko aitaka CWT kuendana na kasi ya mabadiliko duniani

    October 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa