Ili uweze kumuona Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe.Adam Kighoma Malima Ofisini kwake mambo yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:-
1.Anza kupeleka hoja yako au shida yako kwa Mkuu wa Wilaya unayoishi.Endapo tatizo lako litakuwa bado halijashughulikiwa ipasavyo,Mkuu wa Wilaya anaweza kukushauri umuone Mkuu wa Mkoa au wewe mwenyewe unaweza kuja kumuona Mkuu wa Mkoa.Ukifika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
i) Onana na Katibu Mutashi wa Mkuu wa Mkoa.Katibu Mutashi atakuombea nafasi ya kumuona Katibu wa Mkuu wa Mkoa. Katibu wa Mkuu wa Mkoa atakusikiliza na endapo anaweza kushughulikia swala lako atalimaliza yeye
mwenyewe lakini kama ataona hadi Mkuu wa Mkoa ndiyo ataweza kulimaliza tatizo lako atawasiliana na Mkuu wa Mkoa na atakuombea nafasi ya kumuona Mkuu wa Mkoa.
ii) Baada ya kuwasilisha malalamiko yako unashauriwa ujadiliane na katibu wa Mkuu wa Mkoa ili kuweza kufuatilia utekelezaji wa kile mlichoshauriana na Mkuu wa Mkoa
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: P.o.Box 299 Musoma
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa