• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TISEZA yazindua dawati la uwekezaji Mara

Posted on: January 27th, 2026

Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) leo tarehe 26 Januari, 2026 imefanya semina na wadau wa uwekezaji katika Mkoa wa Mara kwa ajili ya kuhamasisha uwekezaji katika sekta mbalimbali za kiuchumi zilizopo hapa nchini na imezindua rasmi Dawati la Uwekezaji la Mkoa wa Mara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dawati la Uwekezaji Mkoa wa Mara, Mwenyekiti wa Bodi ya TISEZA Balozi Dkt. Aziz Mlima amesema mamlaka hiyo inalenga kuwawezesha Watanzania kutumia fursa za uwekezaji kwa kuwapa unafuu wa mitaji kutokana na punguzo la kodi na ushuru wa forodha.

“Lengo la Serikali ni kuongeza idadi ya wawekezaji ili kutekeleza Dira ya 2050 ambayo inalenga kukuza uchumi wa Tanzania kufikia Dola za Kimarekani zaidi ya Trilioni 1 kwa kuongeza wawekezaji wa ndani” amesema Dkt. Mlima.  

Dkt. Mlima amesema Serikali imechukua hatua za makusudi kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwahamasisha Watanzania zaidi kushiriki katika uwekezaji kwa kuwapa misamaha ya kodi na punguzo la ushuru wa forodha kwa baadhi ya bidhaa zinazotumika katika miradi ya uwekezaji jambo ambalo amesema linalenga kuchochea wawekezaji zaidi.  

Dkt. Mlima pia amempongeza Mwekezaji wa Mkoa wa Mara Ndugu Emille Gotham kwa kuanzisha mchakato wa kuwekeza katika uzalishaji wa chakula cha samaki MKoa wa Mara na kumhakikishia kuwa soko la uhakika kutokana na serikali kuwahamasisha wananchi kufuga samaki katika vizimba na kwa sasa chakula hicho kinatoka nje ya Tanzania.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Uhamasishaji Uwekezaji TISEZA Ndugu Geore Mukono amesema  kuwa kampeni hiyo itaonyesha fursa mbalimbali zilizopo katika mikoa, taratibu za usajili wa miradi ya uwekezaji kwa lengo la kupata vyeti vya uwekezaji na leseni katika maeneo maalum ya kiuchumi, vivutio vya kikodi na visivyo vya kikodi vinavyotolewa kwa wawekezaji hapa nchini.

Ndugu Mukono amesema wawekezaji watakaojisajiri watakapa unafuu wa ushuru wa forodha hadi asilimia 100 na msamaha wa kodi hadi asilimia 75 katika vifaa vinavyotumika katika uwekezaji baada ya mradi husika kusajiliwa.

Ndugu Mukono ametolea mfano wawekezaji katika ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba wanaweza kupata msamaha wa kodi hadi asilimia 75 katika ununuzi wa maboti, injini, ndoano, magari ya kusafirishia samaki, vizimba, neti na kadhalika.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Ndugu Gambaless Timotheo amesema ameishukuru TISEZA kwa kuhamasisha uwekezaji katika Mkoa wa Mara na kuwataka wafanyabiashara na taasisi za kifedha kushirikiana kuanzisha miradi ya uwekezaji.

Ndugu Gambales ameishukuru TISEZA kwa kuzindua Dawati la Uwekezaji Mkoa wa Mara na kuahidi kuwa Mkoa wa Mara utawasaidia Watanzania wanaotaka kuwekeza kupata taarifa na msaada watakaohitaji.

Kwa upande wake, Mfanyabiashara Annastazia Omollo Mkazi wa Manispaa ya Musoma ameitaka TISEZA kupeleka fursa za uwekezaji katika maeneo ya vijijini ili wananchi wengi zaidi waweze kuzisikia na kuchangamkia fursa hizo.

“Wananchi wengi wa vijijini wanakosa fursa za kiuchumi kwa sababu ya kutofikiwa na programu mbalimbali za Serikali na wadau zinazotolewa “ amesema Ndugu Omollo na kuishauri TISEZA kuhakikisha wananchi waliopo vijijini wanapata fursa hiyo.

Ndugu Omollo amesema vijijini kuwa wakulima na wafugaji wengi wenye mashamba makubwa na wanaomiliki idadi kubwa ya mifugo ambao wakipata elimu watafanya shughuli zao kisasa na kuwekeza zaidi katika shughuli zao na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na TISEZA na taasisi nyingine.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chemba ya Bishara Mkoa wa Mara Ndugu Denis Nyakisinda amesema taasisi hiyo imeandaa tukio la kukutana kati ya Wafanyabiashara wa Mkoa wa Mara na watendaji wa taasisi zote za Serikali litakalofanyika mwezi Februari, 2026 kna kuwataka wafanyabiashara wote kujitokeza kushiriki tukio hilo.

Aidha, Ndugu Nyakisinda amesema kuwa taasisi hiyo inaandaa kongamano la Wafanyabiashara Mkoa wa Mara hivi karibuni na kuwataka wafanyabiashara wa Mkoa wa Mara kujiunga na taasisi hiyo na kushiriki matukio hayo ili kupata taarifa.

Semina hiyo ni sehemu ya Kampeni ya Kitaifa ya Uhamasishaji Uwekezaji wa Ndani iliyoanza tarehe 18 Januari, 2026 hadi tarehe 09 Aprili, 2026 itaendeshwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na imeanza kutekelezwa katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwa na Kauli mbiu ”Unawezeshwa Kuwekeza kwa kupewa Unafuu wa Mtaji”

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • TISEZA yazindua dawati la uwekezaji Mara

    January 27, 2026
  • TISEZA yahamasisha uwekezaji katika fursa za Mkoa wa Mara

    January 24, 2026
  • Mtambi afanya ziara Butiama

    January 20, 2026
  • Kanali Mtambi ahimiza upandaji miti

    January 14, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa