MKUU WA MKOA - MARA AKIPOKEA MWENGE WA UHURU TOKA MKUU WA MKOA - MWANZA
KATIBU TAWALA (M) WA SIMIYU BW. JUMANNE SAGINI AKICHAGIA KWENYE KIKAO CHA PIC
MHE. MKUU WA MKOA AKIWA NA UGENI WA GRACA MACHEL TRUST FUND
MKUU WA MKOA WA MARA AKILA KIAPO
MHE. MKUU WA MKOA AKIWA KWENYE PICHA YA PAMOJA NA WAKUU WA WILAYA
UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MWL. NYERERE
NYUMBU WAKIVUKA MTO MARA

MWENGE WA UHURU WAANZA MBIO ZAKE MKOANI MARA

Mwenge wa Uhuru umeanza mbio zake Mkoani Mara ambapo utakimbizwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa tisa (9) katika tarehe 14 Agosti 2016 hadi tarehe 19 Agosti 2016. Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2016 ni “Vijana ni Nguvukazi ya Taifa”, wenye kauli mbiu “Washirikishwe na Kuwezeshwa’’. Ili kusoma MAELEZO MAFUPI KWA KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE WA UHURU YALIYOTOLEWA NA MHE. DKT. CHARLES O. MLINGWA MKUU WA MKOA WA MARA WAKATI WA KUPOKEA MWENGE WA UHURU KUTOKA KWA MKUU WA MKOA WA MWANZA TAREHE 14/08/2016, Bonyeza hapa.

KARIBU MKOA WA MARA

MAHALI MKOA ULIPO: Mkoa wa Mara una eneo la ukubwa wa Kilomita za Mraba zipatazo 30,150. Mkoa una jumla ya wakazi 1,743,830 kwa mujibu wa Sensa ya watu na makazi iliyofanyika mwaka 2012. Mtawanyiko wa watu ni watu 61 kwa kila kilomita moja ya eneo. Jina la Mkoa wa Mara limetokana na Mto Mkuu wa Mara ambao umeanzia maeneo ya nchi jirani ya Kenya na kutiririsha maji yake kwa kupitia Wilaya za Serengeti, Tarime, Musoma Vijijini hadi Ziwa Victoria. Mkoa upo upande wa Kaskazini mwa Tanzania ambapo kwa upande wa Kaskazini Mkoa umepakana na Nchi za Kenya na Uganda, upande wa Mashariki ni Mkoa wa Arusha, upande wa Kusini ni Mkoa wa Shinyanga, upande wa Kusini-Magharibi ni Mkoa wa Simiyu na upande wa Magharibi ni Mkoa wa Kagera ukiwa usawa wa Ziwa Victoria. Mkoa upo kwenye latitudes 10 0’ na 20 31’, Kusini mwa Ikweta na katikati ya longitudes 330 10’ na 350 15’, Mashariki mwa Griniwichi

Eneo la Mkoa wa Mara ni Kilometa za mraba 30,150. Eneo la Kilometa mraba 10,584 ni eneo lenye maji ya Ziwa Victoria na kilometa za mraba 9,842 ni eneo la Hifadhi ya Taifa ya mbuga za wanyama ya Serengeti, sawa na 32.6% ya eneo lote la Mkoa wa Mara ambayo ni sehemu inayotambuliwa kuwa ni maajabu makuu ya Dunia.

UTAWALA:Mkoa umegawanyika katika wilaya sita (6) za Musoma, Butiama, Bunda, Serengeti, Tarime na Rorya na Halmashauri kumi (10) ambazo ni Bunda (W), Butiama , Musoma (W), Musoma Manispaa, Rorya (W),Bunda Mji, Serengeti (W), Tarime (W), Tarime Mji, Mugumu-Mji mdogo. Tarafa 20 Kata 182, Vijiji 479, Mitaa 287, Vitongoji 2,543. Bonyeza hapa kupata jedwali la IDADI KATA, MITAA, VIJIJI NA VITONGOJI KATIKA MKOA WA MARA.

. KARIBU MBUGA YA TAIFA YA SERENGETI ILI KUJIONEA MAKUNDI YA WANYAMA NA NDEGE.

VIKAO VYA BODI YA BARABARA NA KAMATI YA USHAURI MKOA VYAFANYIKA NA KUAZIMIA MAMBO YA MAENDELEO

.MWONGOZO WA BAJETI MWAKA 2016

.SHERIA YA BAJETI NA KANUNI ZAKE