• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC Mtanda aendelea na ziara Wilaya ya Bunda

Posted on: September 22nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo ameendelea na ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo ametembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na kuagiza kupatiwa taarifa ya ukaguzi iliyofanywa na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kuhusu matumizi ya fedha katika ujenzi wa hospitali hiyo.

Akizungumza katika hospitali hiyo Mhe. Mtanda ameahidi kuwachukulia hatua watumishi wote watakaotajwa kukiuka taratibu, uzembe au kuiba fedha katika ujenzi wa hospitali hiyo.

“Watu wote waliohusika kwa namna mmoja au nyingine nitahakikisha wanawajibishwa kwa mujibu wa sheria haraka iwezekanavyo” amesema Mhe. Mtanda na kumtaka Mkurugenzi kukamilisha kwa haraka majengo yanayoendelea kujengwa ili kupanua huduma katika hospitali hiyo.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na uongozi wa Kata ya Nyamswa kukamilisha ulipaji wa fidia kwa Bibi Mary Wambura (71) anayedai fidia ya shilingi milioni 22 ili kuhama katika nyumba yake iliyopo ndani ya eneo la hospitali hiyo. 

Tayari, Kata ya Nyamswa imemjengea nyumba mbadala ya kuhamia katika eneo jingine lakini makubaliano yalikuwa alipwe pia fidia hiyo kwa ajili ya mashamba yake ili ahame kupisha mradi wa hospitali hiyo makubaliano ambayo hayajakamilishwa tangu mwaka 2009.  

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara amewataka wananchi wa eneo la Mariwanda kuwa makini wakati wa kuchagua kaya zitakazonufaika na Mpango wa Kaya Maskini (TASAF) ili wanufaika wote wa mfuko huo wawe na sifa za kuwezesha kunufaika na TASAF.

Aidha, amewataka Watendaji wa Vijiji, Kata na mratibu wa TASAF wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda  kuhakikisha kuwa watu wote wanaostahili kuwemo kwenye mpango huo wanakuwemo na wasiostahili wanaondolewa.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa amezungumza na wananchi katika eneo la Mariwanda na kukagua mradi wa maji eneo la Mariwanda, miradi ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, Shule za Sekondari za Mariwanda na Tirina katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

 Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bunda, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya na wawakilishi wa Makatibu Tawala wasaidizi sehemu za Elimu na Miundombinu, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi wa Halmashauri,  baadhi ya watumishi wa Halmashauri na taasisi zilizopo katika Wilaya ya Bunda.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya awataka wahanga kutumia misaada kuboresha maisha

    May 19, 2025
  • BASATA yaijengea uwezo Mkoa wa Mara

    May 15, 2025
  • Mara kutumia fursa zilizopo kuboresha sanaa kwa vijana

    May 15, 2025
  • RC aipongeza Musoma ushindi wa ubora wa huduma za afya Kitaifa

    May 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa