• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC awapokea Maafisa na wanafunzi kutoka Chuo cha Jeshi cha CSC

Posted on: October 13th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evance Alfred Mtambi leo tarehe 13 Oktoba, 2025 amewapokea wakufunzi, Maafisa na wanafunzi 48 kutoka Chuo cha Ukamanda na Unadhimu (CSC) kilichopo Duluti, Mkoani Arusha waliopo katika Mkoa wa Mara kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mhe. Mtambi amewakaribisha Maafisa na Wanafunzi hao katika Mkoa wa Mara na kuwahakikishia kuwa Mara ipo salama na wananchi wake wanaendelea kufanya shughuli zao za kila siku.

“Kwa niaba ya wananchi na viongozi wa Mkoa wa Mara ninawakaribisha Maafisa na wanafunzi wote wa Chuo hiki katika Mkoa wa Mara na ninawaomba kuangalia uwezekano wa kutembelea eneo la Fort Ikoma ambapo mafunzo ya kijeshi yalipoanzia katika historia ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).   

Mhe. Mtambi amewataka viongozi, watedaji na wananchi wa Mkoa wa Mara kuwapa ushirikiano Maafisa na Waafunzi hao kwa muda wote watakaokuwepo katika Mkoa wa Mara na kuwataka viongozi wa msafara huo kutoka taarifa kama watapata changamaoto yoyote katika mafunzo yao.  

Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara umechaguliwa kufanyiwa mafunzo hayo kutokana na kuwa ni rasilimali za kiuchumi ikiwemo Ziwa Victoria, mito, madini, maeneo ya kilimo, ufugaji na maeneo ya kihistoria ya nchi ya Tanzania.

Aidha, Kanali Mtambi amesema Mkoa wa Mara upo katika eneo la kimkakati na unapakana na nchi za Kenya na Uganda na hivyo kuwa sehemu muhimu ya biashara za mpakani na biashara za ndani ya nchi kutokana na eneo lake.

Mhe. Mtambi amewataka maafisa na wanafunzi hao kuwa mabalozi wa Mkoa wa Mara na kuwataka kusaidia kuyatangaza mambo mazuri ya Mkoa wa Mara popote watakapoenda baada ya mafunzo hayo.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Mafunzo wa CSC Kamali Verious C. Mbuzi amesema wapo katika Mkoa wa Mara kwa mafunzo kwa vitendo ya wiki moja kujifunza kuhusiana na miundo msingi ya kiuchumi na usalama wa nchi kuanzia leo tarehe 13 Oktoba, 2025 hadi tarehe 18 Oktoba, 2025.

Kanali Mbuzi amesema katika mafunzo kwa vitendo maafisa na wanafunzi wa chuo hicho  wamegawanyika katika makundi matatu na wanafanya mafunzo kwa vitendo katika mikoa ya Mara, Iringa na Kigoma.

Kanali Mbuzi amesema Chuo hicho kinatoa kozi za Shahada ya Umahiri na Diploma na wanafunzi wanaoandaliwa kubeba majukumu makubwa na wanatokea katika nchi za Burundi, Rwanda, Uganda, Afrika Kusini, Zimbabwe, Malawi, Zambia, Namibia na wenyeji Tanzania wakati wakufunzi waliomo katika msafara huo wanatoka katika mataifa ya India, Zimbabwe, Zambia na Tanzania na amekabidhi zawadi mbalimbali kutoka katika Chuo hicho kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara. 

Ameyataja maeneo yatakayotembelewa katika ziara hiyo kuwa ni pamoja na Manispaa ya Musoma, Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, shughuli za Kilimo, Ufugaji wa samaki kwenye vizimba, Chuo Kikuu cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Butiama na Makumbusho ya Mwalimu Nyerere Butiama.

Hafla ya mapokezi hayo imehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka, wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa, wajumbe wa Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa.

Baada ya mapokezi hayo, Maafisa na Wanafunzi hao wamekutana na viongozi na maafisa kutoka Manispaa ya Musoma katika Ukumbi wa Uwekezaji, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kabla ya kuendelea na ziara yao.  


Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC awapokea Maafisa na wanafunzi kutoka Chuo cha Jeshi cha CSC

    October 13, 2025
  • RC awapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 Mara

    October 13, 2025
  • Mtambi aipongeza CDEA kwa kuanzisha Redio Butiama FM

    October 03, 2025
  • Mtambi awataka wajasiriamali kuwa na nidhamu ya fedha

    October 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa