• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Nyansaho ahaidi kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kimkakati

Posted on: December 24th, 2025

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho leo tarehe 21 Disemba, 2025 ametembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na kuahidi kushirikiana na wabunge na viongozi wengine wa Mkoa wa Mara kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kimkakati na miradi iliyopo katika ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2025-2030.

Mhe. Nyansaho ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na viongozi na watendaji wa Mkoa wa Mara walioshiriki mapokezi hayo kufuatia maombi yaliyotolewa kwa nyakati tofauti na Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara na kuwawahakikishia wananchi kuwa miradi yote iliyomo kwenye ilani ya CCM itatekelezwa mapema iwezekanavyo.

“Sisi tutajitahidi kuhakikisha kuwa miundombinu ya kimkakati ya Mkoa wa Mara inapata fedha za utekelezaji na miradi inakamilika kwa wakati” amesema Mhe. Nyansaho na kuongeza kuwa anafuatilia kwa karibu miradi ya barabara za ndani ya Mkoa na ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti.

Aidha, Mhe. Dkt. Nyansaho ametembelea ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara na kuzungumza na Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Mhe. Patrick Chandi Marwa.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mhe. Nyansaho, Mhe. Chandi amesema Mkoa wa Mara upo salama na haukuathirika sana na vurugu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kutokana na jitihada zilizochukuliwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara.

Mhe. Chandi amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Mara kwa kushiriki uchaguzi na kuwachagua viongozi wa Chama cha Mapinduzi katika nafasi za Urais na Ubunge na kuufanya Mkoa wa Mara kuwa kati ya mikoa 10 ya Tanzania iliyofanya vizuri katika uchaguzi huo.  

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amemuomba Mhe. Waziri kusaidia kufanikisha utekelezaji wa miradi ya barabara ya Musoma-Arusha, barabara za ndani ya Mkoa, upanuzi na ukarabati wa Uwanja wa Ndege Musoma na Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Serengeti miradi ambayo amesema itaimarisha huduma na uchumi wa Mkoa wa Mara na Taifa kwa ujumla.

Mhe. Mtambi amesema Mkoa upo salama na amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Mara kwa namna ambavyo wameulinda Mkoa wao na watu wake kwa amani na utulivu katika mwaka 2025 na kuwataka kuendelea kufanya hivyo kwa mwaka 2026.

 Mapokezi hayo yalihudhuriwa na viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Menejimenti ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Musoma, viongozi wa dini.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi yaingia Mara

    January 08, 2026
  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa