• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi awataka wananchi kushiriki maadhimisho ya siku ya kupinga ukatili kwa wazee

Posted on: June 11th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo amezungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kutoa taarifa ya Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee ambayo kitaifa yatafanyika katika Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara tarehe 15 Juni, 2025.

“Ninaomba kuchukua fursa hii kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Mara na Mikoa ya jirani kushiriki maadhimisho haya muhimu ambayo kitaifa yatafanyika katika Shule ya Msingi Miembeni, Halmashauri ya Mji wa Bunda” amesema Mhe. Mtambi.  

Mhe. Mtambi amesema mgeni rasmi katika maadhimisho haya atakuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dorothy Gwajima na kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka 2024 ni “Utu, Usalama na Ustawi ni nyenzo ya Kutokomeza Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wazee”

Mhe. Mtambi amesema kuwa maadhimisho haya yatatanguliwa na mashindano ya michezo baina ya wazee itakayofanyika tarehe 13 Juni, 2024 katika Chuo cha Ualimu Bunda, kongamano kuhusu masuala mbalimbali ya wazee litakalofanyika Chuo cha Ualimu Bunda na wazee kwenda kutembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwitongo, Butiama tarehe 14 Juni, 2024.

Aidha, kwa siku zote tatu (tarehe 13-15 Juni, 2024) kutakuwepo na upimaji wa afya bure na maonyesho mbalimbali ya shughuli za wazee na kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 15 Juni, 2024 katika viwanja vya Shule ya Msingi Miembeni.  

Kwa mujibu wa Mhe. Mtambi Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee yameanza kuazimishwa kimataifa mwaka 2011 baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kuzitaka nchi wanachama kuazimisha siku hiyo.

Mhe. Mtambi amesema malengo ya maadhimisho haya ni kutoa elimu, kubadili mitizamo ya jamii kuhusiana na wazee na kuzeeka na kuwasaidia wazee kupata sehemu ya kusemea kero zao zinazowakabili katika jamii.

Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara hauna matukio ya kuwanyanyasa wazee na maadhimisho haya yameletwa ili watu wa mikoa mingine wajifunze namna nzuri ya kuishi na kuwatumia wazee kwa ajili ya kutatua changamoto zinazowakabili.

Mhe. Mtanda amesema maandalizi kwa ajili ya maadhimisho hayo yamekamilika na kuwataka wananchi kujitokeza kupata elimu na kuwapeleka wazee kupima afya zao bure katika muda wote wa siku tatu za  maadhimisho hayo.  

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Wananchi Rorya wahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia

    August 19, 2025
  • Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa awasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61

    August 18, 2025
  • Mwenge wakagua miradi ya bilioni 6 Musoma

    August 18, 2025
  • Maambukizi ya UKIMWI katika Wilaya ya Bunda yamepungua

    August 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa