• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi awataka wananchi kuchangamkia fursa ya kupima saratani bure

Posted on: December 4th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 04 Disemba, 2025 amewapokea madaktari bingwa wa Saratani kutoka Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na Taasisi ya Global Medicare waliopo katika Mkoa wa Mara kwa ajili ya uchunguzi wa magonjwa ya saratani yatakayofanyika kuanzia kesho tarehe 5 Disemba, 2025 hadi tarehe 7 Disemba, 2025 katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mhe. Mtambi amewataka wananchi wa Mkoa wa Mara na mikoa jirani kujitokeza kwa wingi katika muda uliopangwa ii kupata huduma na ushauri kuhusu dalili za magonjwa ya saratani kutoka kwa madaktari bingwa wa saratani ambazo zitatolewa bila malipo yoyote.

“Wakiwa katika Hospitali ya Serengeti, wataalamu hawa watatoa huduma ya upimaji wa saratani kwa wananchi, matibabu ya awali, ushauri kuhusiana na matibabu na rufaa kwa wagonjwa watakaogundulika” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema hii ni mara ya kwanza kwa wataalamu wabobezi wa magonjwa ya saratani kwenda katika Wilaya ya Serengeti na hivyo kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao huku akiwasistiza kuwa afya ni mtaji katika maendeleo yao.

Mhe. Mtambi ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa namna wanavyowajali wananchi wa Mkoa wa Mara kwa kuwaletea wataalamu bingwa kwa ajili ya kuwafanyia vipimo vya saratani bure katika Wilaya ya Serengeti.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Kinga, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dkt. Crispin Kahesa amesema wataalamu hayo wapo katika Mkoa wa Mara kwa ajili ya kuwasaidia wananchi kufanya uchunguzi wa saratani kwa makundi mbalimbali.

Dkt. Kahesa amesema kuwa wataalamu hao watafanya uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi kwa wanawake, kwa wanaume saratani ya tezi dume kwa kutumia damu na watatoa ushauri kwa wananchi na kuongeza kuwa timu ya wataalamu hao imejipanga na imekuja na inamchanganyiko wa madaktari, wachunguzi wa maabara, wauguzi na washauri waliojikita katika kutoa elimu.

Dkt. Kahesa amesema watu ambao watagundulika kuwa na dalili za awali za saratani watapewa tiba na wale ambao wanaungonjwa wa saratani watapewa rufaa kwa ajili kwenda katika Hospitali za Taifa ili waweze kupata matibabu.

Dkt. Kahesa amesema kwa Tanzania kila mwaka wanapata wagonjwa 42,000 wapya na kati ya hao asilimia 30 wanatoka katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na Mkoa wa Mara ukiwa ni miungoni mwa mikoa imeathirika na kuwataka wananchi wa Mara kujitokeza kwa wingi kwenda kupima.  

Amesema kwa sasa Tanzania imejipanga sana kutibu wagonjwa wa saratani ambao hapo awali walikuwa wanapelekwa nje ya nchi lakini kwa sasa wanatibiwa hapa nchini kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali ili kuimarisha afya za wananchi.

“Kwa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, katika kipindi cha miaka minne Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 60 zimewekezwa na zimesaidia kuanzisha tiba utalii na kukkifanya kituo cha tiba kwa kanda ya Kusini mwa Afrika” amesema Dkt. Kahesa.  

Mapokezi hayo yamehudhuliwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya, maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na Taasisi ya Global Medicare na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mtambi awataka wananchi kuchangamkia fursa ya kupima saratani bure

    December 04, 2025
  • DC Chikoka afungua semina ya michongo kwa maafisa usafirishaji Musoma

    December 03, 2025
  • RC Mtambi awataka viongozi wa dini kuwahamasisha wananchi kuilinda Tanzania

    December 01, 2025
  • Kusaya aridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa ofisi za Hazina Ndogo Mara

    November 27, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa