• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi awataka wajasiriamali kuwa na nidhamu ya fedha

Posted on: October 1st, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 2 Oktoba, 2025 amefunga Kongamano la wafanyabiashara ndogondogo Mkoa wa Mara lililofanyika katika ukumbi wa MCC, Manispaa ya Musoma na kuwataka kuwa na nidhamu ya fedha ili kuweza kutajirika.

Akizungumza wakati akifunga kongamano hilo, Mhe. Mtambi amesema wakiwa na nidhamu ya fedha wataweza kuchukua mikopo na kuirejesha kwa uaminifu na kwa wakati jambo ambalo linaweza kuwajengea uwezo wa kupata fedha nyingi zaidi.

“Duniani kote matajiri wakubwa walianza kama wajasiriamali na kutokana na nidhamu ya matumizi ya fedha wakakua hadi kuwa matajiri wakubwa sana” amesema Mhe. Mtambi na kuongezea kuwa ujasiriamali ni kazi rasmi na kazi zote zinahitaji nidhamu ili uweze kufanikiwa.

Mhe. Mtambi amesema wakiwa na nidhamu ya matumizi ya fedha itawasaidia kuweza kukuza mitaji yao kwa kudunduliza fedha kidogo wanazopata pamoja na kutumia kwa weredi mikopo wanayochukua ili kuwaletea manufaa yanayotarajiwa na hivyo itawawezesha kukua kiuchumi.

Mhe. Mtambi ameitaka Benki ya NMB kuongeza kasi ya kushughulikia mikopo ya wajasiriamali na kuwasilisha taarifa ofisini kwake kila mwezi kuhusiana na idadi ya wajasiriamali walioomba mikopo na waliopewa mikopo kwa kutumia fedha zilizotolewa na Serikali kwa wajasiriamali wadogo.

Kanali Mtambi amezitaka taasisi na wadau wote kuwasaidia wajasiriamali kwa kuwawekea mazingira wezeshi ya kufanya biashara zao na kuwapa mafunzo mbalimbali ili waweze kufanya biashara zao katika mazingira mazuri na kukuza uchumi wao.  

Mhe. Mtambi amewapongeza wanawake wajasiriamali wa Mkoa wa Mara kwa kujitokeza kwa wingi kujisajiri katika mfumo wa kuwatambua wajasiriamali kwa wingi na kuwahamasisha waendelee kujisajiri itawasaidia katika kutambulika kiurahisi na kupata mikopo ya riba nafuu.  

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Ndogondogo Mkoa wa Mara Bwana Charles Waitara amesema lengo la Kongamano hili ni kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri alizozifanya kwenye makundi mbalimbali ya wafanyabiashara ndogondogo katika Mkoa wa Mara.

Bwana Waitara amesema katika kipindi hiki, wafanyabiashara ndogo ndogo 5,086 wamesajiliwa na wamefanikiwa kupata mikopo kupitia Benki ya NMB na jumla ya wanufaika 230 wamepata mikopo hiyo na Halmashauri ya Manispaa ya Musoma imewapatia eneo la kujenga Machinga Complex katika Kata ya Bweri.

Ameyataja mafanikio mengine waliyoyapata ni pamoja na kupungua kwa ada ya leseni na faini za usalama barabarani kwa madereva wa bodaboda na kwa upande wa wakulima wamepata mbolea ya ruzuku, mashamba darasa ya kilimo biashara ya umwagiliaji kwa vijana.

Bwana Waitara ametumia fursa hiyo kueleza changamoto ya kusuasua kwa utoaji wa mikopo ya Serikali inayotolewa kupitia Benki ya NMB katika matawi yote ya benki hiyo yaliyopo nje ya Manispaa ya Musoma.

Kwa upande wake, Mfanyabiashara Nyehita Wilfred Nyehita amesema yeye alianza kuanzia akiwa shule ya msingi kufanya biashara ndogo ndogo na kwa sasa amekuwa mfanyabiashara mkubwa anayekopesheka fedha nyingi kutokana na uaminifu wake katika kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati.

Bwana Nyehita amesema alipoanza biashara zake, alikuwa anakopa pesa kwa walimu wake na kuzirejesha na baadaaye alipokuwa mkubwa alianza kukopa Benki ambayo mpaka sasa anakopa benki hiyo na kutokana na uaminifu wake wa kurejesha ameweza kuaminika.

“Nilianza kukopa shilingi milioni moja na kwa sasa ninakopa zaidi ya milioni 300 kutokana na uaminifu niliouonyesha katika benki hii kwa muda mrefu” amesema Bwana Nyehita na kuwataka wajasiriamali kujitahidi kutunza uaminifu ili waweze kufanikiwa kutimiza malengo yao.

Kwa upande wake, Mratibu wa kongamano hilo Bwana Fidel Baragaye amesema kuwa kongamano hilo limewajumuisha wajasiriamali zaidi ya 500 kutoka Wilaya ya Musoma likiwa na kauli mbiu “Tunawatambua, Tunawathamini na Kuwawezesha”.

Bwana Baragaye amesema kongamano hilo linafuatia ziara ya viongozi wa Kitaifa wa Wafanyabiashara ndogondogo wanaopita mikoa yote hapa nchini na kwa Mkoa wa Mara makongamano mengine mawili yamefanyika katika Miji ya Bunda na Tarime na kulifanya kongamano hilo kuwa la tatu.

Katika kufunga kongamano hilo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na viongozi wa Wilaya na Manispaa ya Musoma, maafisa kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, viongozi wa wafanyabiashara ndogondogo na wajasiriamali.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC awapokea Maafisa na wanafunzi kutoka Chuo cha Jeshi cha CSC

    October 13, 2025
  • RC awapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 Mara

    October 13, 2025
  • Mtambi aipongeza CDEA kwa kuanzisha Redio Butiama FM

    October 03, 2025
  • Mtambi awataka wajasiriamali kuwa na nidhamu ya fedha

    October 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa