• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi aipongeza Nyansaho Foundation kuchangilia bilioni 40 katika maendeleo ya Mara

Posted on: October 1st, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 30 Septemba, 2025 ameipongeza Nyansaho Foundation kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 4 kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika Mkoa wa Mara tangu taasisi hiyo ilipoanzishwa.

Mhe. Mtambi ametoa pongezi hizo katika hafla ya kukabidhi mabasi ya wananfunzi yenye thamani ya shilingi 372 yaliyotolewa na Nyansaho Foundation kwa Shule za Sekondari za Natta, Machochwe na Ngoreme zilizopo katika Wilaya ya Serengeti.

“Mchango mlioutoa umeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya watu wa Wilaya ya Serengeti na Mkoa wa Mara kwa ujumla” na kuongeza kuwa “Serikali inatambua mchango wa sekta binafsi katika maendeleo” amesema Mhe. Mtambi.  

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtambi ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kuweka utaratibu mzuri wa matumizi ya magari hayo ili kuyawezesha kutoa huduma kwa Sekondari nyingi zaidi katika maeneo yao.

Aidha, Mhe. Mtambi kumpongeza mdau mwingine wa maendeleo aliyejitambulisha kama Mhandisi Stanley ambaye ameshiriki hafla hiyo na ambaye ameahidi kuchangia shilingi milioni 10 kwa ajili ya mafuta ya mabasi hayo. 

Wakati huo huo, Mhe. Mtambi amewahamasisha wananchi wa Mkoa wa Mara kushiriki uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025 na kuwapongeza wananchi kwa kuonyesha mwamko mkubwa katika kujiandikisha, kampeni na uchaguzi na kuwataka kushiriki kupiga kura tarehe 29 Oktoba, 2025.

“Uchaguzi ni fursa ya kikatiba muitumie kuwachagua viongozi watakaowasaidia katika kupata maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wananchi kuwa Serikali itahakikisha kuwa uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu na kuwaonya watu wanaopanga kuanzisha taharuki wakati huu wa uchaguzi kuwa Mkoa wa Mara sio sehemu ya kuchezea na kufanyia majaribio ya vurugu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti na muasisi wa Taasisi hiyo Dkt. Rhino Simon Nyansaho amesema taasisi hiyo imetoa magari hayo kufuatia ahadi aliyeitoa katika mahafali ya shule hizo mwaka jana ambazo zilimpatia changamoto mbalimbali ambazo Taasisi hiyo imezitatua.

Changamoto hizo ni tatizo la maji, bweni la wasichana na mifuko ya saruji katika Shule ya Sekondari ya Machochwe na maji, kugharimia kambi ya wanafunzi wa kidato cha sita na saruji mifuko 500 katika Shule ya Sekondari ya Ngoreme.

Dkt. Nyansaho amesema taasisi yake imegharimia wanafunzi 1,200 waliomaliza kidato cha nne kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) na kuongeza kuwa kama mlezi wa Shule ya Sekondari ya Natta amesaidia kutuma maombi ya ufadhili Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) ambalo limeahidi kutoa shilingi milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala la shule hiyo.

Katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya, viongozi wa Wilaya ya Serengeti, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Nyansaho Foundation, Chama cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa Wilaya ya Serengeti.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC awapokea Maafisa na wanafunzi kutoka Chuo cha Jeshi cha CSC

    October 13, 2025
  • RC awapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 Mara

    October 13, 2025
  • Mtambi aipongeza CDEA kwa kuanzisha Redio Butiama FM

    October 03, 2025
  • Mtambi awataka wajasiriamali kuwa na nidhamu ya fedha

    October 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa