• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi aipongeza CDEA kwa kuanzisha Redio Butiama FM

Posted on: October 3rd, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 03 Oktoba, 2025 ameongoza hafla ya ushirikishwaji wa jamii na uhamasishaji wa wadau wa redio ya Butiama FM na kuipongeza taasisi ya Culture and Development East Africa (CDEA) kwa kuianzisha Kituo cha redio katika Wilaya ya Butiama.  

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtambi Mhe. Mtambi amesema redio Butiama itakuwa kichocheo cha maendeleo ya jamii kutokana na faida mbalimbali zinazotokana na uwepo wake ikiwa ni pamoja na kutangaza biashara, tamaduni, utalii na fursa mbalimbali zilizopo katika Wilaya hiyo.

“Ninawapongeza kwa kuanzisha wazo hili na kuendelea kulifanyia kazi bila kukata tamaa mpaka hapa mlipofikia, baada ya matangazo kuanza angalieni uwezekano wa kupanua matangazo yasikike sehemu kubwa zaidi” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka wadau matangazo katika kituo hicho yatakapoanza kukitumia kituo hicho kwa kutangaza shughuli zao na kulipa gharama za uendeshaji wa kituo hicho ili kiendelee kufanyakazi katika Wilaya ya Butiama.

Kanali Mtambi ameitaka Menejimenti ya Kituo cha Redio Butiama FM kuajiri Watangazaji na Waandishi wa Habari wenye ithibati ili waweze kuyatangaza mambo mazuri yaliyopo katika Wilaya ya Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla.

Mhe. Mtambi amewashukuru wadau mbalimbali wanaochangia kwa hali na mali katika uanzishwaji wa kituo hicho akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ubalozi wa Norway na UNESCO na wanajamii wa Butiama.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amesema Mamlaka ya Elimu ya Ufundi (VETA) Mkoa wa Mara imepunguza gharama za madereva wa bodaboda wanaotaka kujifunza udereva kutoka shilingi 70,000 hadi shilingi 30,000 na kuwahamasisha madereva hao kuchangamkia punguzo hilo.

“Serikali imechukua hatua hii kwa kutambua mchango mkubwa wa Maafisa Usafirishaji kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi wa jamii na Taifa kutokana na kuimarisha mzunguko wa fedha, upatikanaji wa usafiri katika baadhi ya maeneo” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka madereva wa pikipiki kuendesha biashara zao kwa kufuata misingi na miiko ya udereva ili kuweza kuokoa maisha ya watu na mali zao na kuwaletea maendeleo binafsi kutokana na biashara hiyo.

Mhe. Mtambi amewakaribisha wananchi wa Mkoa wa Mara kushiriki mapokezi na mikutano ya hadhara ya Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anayetarajia kuwa katika Mkoa wa Mara tarehe 9-10 Oktoba, 2025. 

Aidha, Mhe. Mtambi amewataka wananchi wa Butiama na Mkoa wa Mara kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kuwasilikiza wagombea na kuwachagua viongozi watakaowaongoza katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mhe. Mtambi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Mara kuwa kutokana na hatua zilizochukuliwa na Serikali kurekebisha miundombinu ya kupooza na kusambaza umeme katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa, Suala la kukatika katika kwa umeme litakuwa historia hivi karibuni.

Katika Halfa hiyo, Mkuu wa Mkoa alitoa ahadi ya lita 200 za mafuta ya jenereta la kituo hicho huku mgombea ubunge jimbo la Butiama kupitia Chama cha Mapinduzi Dkt. Wilson Mahera akitoa shilingi 100,000 kwa ajili ya mafuta.

Kwa upande wake, Chifu wa Ukoo wa Burito Nyerere na Mlezi wa Familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Chifu Japhet Wanzagi ameipongeza CDEA kwa kuanzisha Redio Butiama FM na kuileta katika Wilaya ya Butiama.

Chifu Wanzagi amewaomba wadau na wananchi wa Wilaya ya Butiama kukitumia kituo hicho katika kutangaza shughuli, fursa na biashara zao ili kiweze kusaidia kutoa mchango uliokusudiwa wa kuanzishwa kwa kituo hicho.

Aidha, Chifu Wanzagi ameuomba uongozi wa kituo hicho kuweka gharama nafuu za matangazo ili wadau wengi zaidi waweze kukitumia kituo hicho kujitangaza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya CDEA na Butiama Redio FM Ndugu Madaraka Nyerere amesema kuanzishwa kwa redio hiyo kunatokana na ufadhili uliotolewa na UNESCO mwaka 2012 na mpaka sasa wanayo studio na vyombo vya kuendeshea matangazo.

Ndugu Madaraka Nyerere amesema kwa sasa wanategemea Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) watafanya ukaguzi wao ili kutoa leseni ya uendeshaji wa kituo hicho na baada ya hapo matangazo katika kituo hicho yataanza rasmi.

Ndugu Madaraka amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa kuweza kutenga muda na kushiriki na wadau wote walishiriki hafla hiyo kwa na kuwaomba kuchangia kwa hali na mali uendelevu wa kituo hicho.   

 Katika hafla hiyo, Mhe. Mtambi ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Menejimenti ya Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Mgombea ubunge wa Jimbo la Butiama, Familia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambara Nyerere, Viongozi wa CDEA na Butiama FM na wananchi wa Wilaya ya Butiama. 

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC awapokea Maafisa na wanafunzi kutoka Chuo cha Jeshi cha CSC

    October 13, 2025
  • RC awapokea Madaktari Bingwa wa Mama Samia 64 Mara

    October 13, 2025
  • Mtambi aipongeza CDEA kwa kuanzisha Redio Butiama FM

    October 03, 2025
  • Mtambi awataka wajasiriamali kuwa na nidhamu ya fedha

    October 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa