• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kusaya aridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa ofisi za Hazina Ndogo Mara

Posted on: November 27th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo taraehe 27 Novemba, 2025 amefanya ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa ofisi za Hazina Ngogo Mkoa wa Mara iliyopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.

“Nimeangalia vigezo vyote katika ukarabati wa jengo hili, kazi iliyofanyika inaendana na thamani ya pesa iliyotolewa na Serikali kukarabati jengo hili, imefanyika kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa, hongereni sana” amesema Ndugu Kusaya.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa jengo hilo, Ndugu Kusaya amempongeza fundi na wasimamizi wa mradi huo kwa namna walivyosimamia ukarabati wa jengo hilo.

Ndugu Kusaya amekitaka Kitengo cha Manunuzi na Ugavi kukamilisha ununuzi wa vifaa vilivyobakia kwa ubora unaotakiwa na kuwataka kuendelea kutafuta wazabuni zaidi wa kuleta vifaa hivyo katika mikoa ya Mwanza, Dodoma au Dar es Salaam.

Ndugu Kusaya amemtaka fundi aliyepewa kazi ya kukarabati jengo hilo kukamilisha kazi ya ukarabati wiki hii ili wiki ijayo akabidhi mradi huo ili jengo hilo liweze kuanza kutumika.

Wakati huo huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara amekagua ofisi ya madereva na walinzi na kuagiza Sehemu ya Utawala na Rasilimali Watu kufanya maboresho mbalimbali katika ofisi hizo.

Kwa upande wake, Meneja wa mradi huo, Mhandisi Baraka Mwashambwa ameeleza kuwa utekelezaji wa mradi huo mpaka sasa umefikia asilimia 95 na sehemu iliyobakia inasubiria vifaa  vilivyo katika hatua za manunuzi ili kuweza kufunga viyoyozi, mfumo wa Tehama na kufanya usafi.

“Ukarabati wa jengo hili umeanza tarehe 21/08/2025 na ulitegemewa kukamilika tarehe 20/11/2025 lakini umechelewa kutokana na kukosekana kwa vifaa vya kuwezesha kufunga viyoyozi, mfumo wa Tehama” amesema Mhandisi Mwashambwa.

Akizungumza katika ukaguzi huo, Mkuu wa Hazina Ndogo Mkoa wa Mara Ndugu Abubakar Shija Machalo ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa utekelezaji wa mradi huo kwa wakati kama ilivyokuwa imepangwa.

“Nitoe shukrani za dhati kwako Katibu Tawala wa Mkoa na Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara kwa jitihada ulizozifanya mpaka hatua ya mradi ilipofikia na kulingana na maelekezo yako, wiki ijayo tunategemea kurejea na kuanza kufanyia kazi katika jengo hili” amesema Ndugu Machalo.

Aidha, Ndugu Mashalo amempongeza mkandarasi na Meneja mradi kwa kutekeleza mradi huo kwa wakati na uaminifu kukmilisha mradi huu.

Ukarabati wa Ofisi ya Hazina Ndogo Mkoa wa Mara unatekelezwa kwa mfumo wa force account na unasimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambayo ndio inamiliki wa jengo hilo, kwa gharama ya shilingi 127,369,360.80.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya aridhishwa na maendeleo ya ukarabati wa ofisi za Hazina Ndogo Mara

    November 27, 2025
  • Kusaya aongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi

    November 26, 2025
  • Mtambi awataka wakandarasi Mara kutekeleza miradi usiku na mchana

    November 08, 2025
  • Mtambi: Jitokezeni kupiga kura

    October 29, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa