• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kusaya aongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi

Posted on: November 26th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo ameongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji na kuwataka Makatibu Tawala wa Wilaya kuzisimamia Halmashauri kuendesha vikao vya mabaraza ya wafanyakazi kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya Serikali.

Ndugu Kusaya ametoa agizo hilo baada ya kupokea taarifa kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE) kuhusiana na baadhi ya Halmashauri kuendesha vikao vya mabaraza ya wafanyakazi bila kuzingatia taratibu na miongozo ya uundaji na uendeshaji wa mabaraza hayo.

“Makatibu Tawala wa Wilaya simamieni mabaraza ya wafanyakazi katika Halmashauri mnazozisimamia ili kuhakikisha mabaraza hayo yanaendeshwa kwa kufuata taratibu na miongozo ya uendeshaji wake” amesema Ndugu Kusaya.

Ndugu Kusaya amemwagiza Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Utawala kuziandikia barua Halmashauri zote za Mkoa wa Mara na kuzitaka ziwasilishe ratiba ya mabaraza ya Wafanyakazi ili aweze kushiriki katika vikao vya mabaraza ya wafanyakazi katika Halmashauri hizo.

Aidha, Ndugu Kusaya amewataka wajumbe wa kikao hicho kutekeleza maazimio yaliyofikiwa katika  kikao na kuwataka kuwaelimisha watumishi wengine kuhusiana na masuala mbalimbali yaliyojadiliwa katika kikao hicho.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Mkoa wa Mara Ndugu John Bomani amempongeza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kwa namna Mkoa unavyoendesha vikao vya Baraza la Wafanyakazi na kumuomba kufuatilia uendeshaji wa mabaraza ya wafanyakazi katika Halmashauri za Mkoa wa Mara.

“Baadhi ya Halmashauri kuna kasoro katika uundaji na uendeshaji wa mabaraza ya wafanyakazi yanakiuka taratibu za kisheria za uanzishwaji na uendeshaji wa mabaraza hayo” amesema Ndugu Bomani.

Ndugu Bomani pia amewataka wajumbe wa kikao hicho kushiriki kikamilifu mchakato wa uchaguzi mkuu wa TUGHE unaotegemewa kuanza hivi karibuni ili kupata viongozi watakaokiongoza chama hicho na kusimamia maslahi ya wafanyakazi.  

Akitoa elimu kuhusiana na UKIMWI na magonjwa yasiyoambukizwa mahala pa kazi, Mratibu wa UKIMWI, Homa ya Ini na Magonjwa ya Ngono Mkoa wa Mara Dkt. Edibily Mtatiro amewahamasisha wajumbe wa kikao hicho kupima na kupata chanjo za homa ya ini ili kuweza kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo.

“Ugonjwa huu sio maarufu sana katika jamii japokuwa unasababisha vifo vingi kutokana na kuambukizwa kwa kutumia njia nyingi na mgonjwa anaugua na kufariki ndani ya muda mfupi” amesema Dkt. Mtatiro.

Dkt. Mtatiro amewahamasisha wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kupima afya zao na kupata chanjo ya homa ya ini mapema kabla ya kupata maambukizi kwani baada ya kuambukizwa hamna dawa ya kutibu ugonjwa huo isipokuwa kuna dawa za kupunguza makali tu.   

Akizungumzia kuhusu magonjwa yasiyoambukizwa Dkt. Mtatiro amewahamasisha wajumbe kula mlo kamili wenye vyakula vya wanga, mboga mboga na matunda kwa kiasi kulingana na shughuli wanazofanya kwa wakati huo.

Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kimehudhuriwa na Wakuu wa Sehemu, Wakuu wa Vitengo, Makatibu Tawala wa Wilaya, Mwenyekiti wa TUGHE Mkoa wa Mara na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambao ni wajumbe wa kikao hicho.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kusaya aongoza kikao cha Baraza la Wafanyakazi

    November 26, 2025
  • Mtambi awataka wakandarasi Mara kutekeleza miradi usiku na mchana

    November 08, 2025
  • Mtambi: Jitokezeni kupiga kura

    October 29, 2025
  • RC Mtambi: Mara ni salama, twendeni tukapige kura

    October 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa