• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Katibu Tawala Mkoa aridhishwa na ukarabati wa majengo

Posted on: September 29th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo tarehe 29 Septemba, 2025 amekagua ukarabati wa ofisi za Hazina Ndogo Mkoa wa Mara na makazi ya Mkuu wa Mkoa unaotekelezwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na kuridhishwa na kazi zinavyoendelea.

Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Ndugu Kusaya amesema hatua za ukarabati zilizofikiwa katika miradi hiyo ni nzuri ukilinganisha na mikataba ambayo ofisi yake iliingia na mafundi kuhusiana na ukarabati huo na kuwataka mafundi kukamilisha kazi yao mapema iwezekanavyo.

“Utekelezaji wa ukarabati huu umefanyika kwa wakati na ubora unaotakiwa, lakini sasa niwaombe tukamilishe kazi haraka ili majengo haya yaweze kutumika kwa shughuli zinazotarajiwa” amesema Ndugu Kusaya.

Akizungumza katika mradi wa ukarabati wa ofisi za Hazina, Ndugu Kusaya ameagiza wasimamizi wa mradi huo kuyafanyia usafi mazingira ya mradi ili kuondoa mawe, vifusi, mbao na vitu vingine ambavyo havihitajiki ili kuwawezesha mafundi kuweza kupita kwa urahisi na kuboresha mazingira ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Aidha, Ndugu Kusaya ameagiza Kitengo cha Manunuzi kufuatilia utengenezaji wa milango na madirisha ya jengo hilo ili kazi ya ukarabati iweze kukamilika kwa wakati.

Akizungumza katika makazi ya Mkuu wa Mkoa, Ndugu Kusaya ameridhishwa na kasi ya ukarabati wa makazi hayo unaoendelea na kuagiza kuitwa wataalamu kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) ili kuweka vizuri nyaya za umeme na mawasiliano katika makazi hayo.  

Kwa upande wake, Mkuu wa Hazina Ndogo, Mkoa wa Mara Bwana Abubakar Shija Machalo amepongeza ushirikiano unaotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika ukarabati na upanuzi wa ofisi hiyo na kuahidi kufuatilia suala la mtaalamu wa mifumo kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ili atoe maelekezo ya kitaalamu.  

Bwana Machalo ameitaka Kamati inayosimamia utekelezaji wa mradi huo kuandaa taarifa ya utekelezaji wa mradi ili iweze kuwasilishwa Hazina ikiwa ni sehemu ya masharti ya makubaliano ya mkataba wa ukarabati wa jengo hilo kati ya Hazina na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Awali akitoa taarifa za ukarabati wa jengo la Hazina Ndogo, Meneja wa Mradi huo Mhandisi Baraka Mwashambwa amesema ofisi hizo zimeanza kukarabatiwa siku 37 zilizopita kwa mkataba wa siku 90 kwa gharama ya zaidi ya shilingi milioni 127 na ukarabati huo unatumia mfumo wa force account.

Mhandisi Mashambwa amesema kwa sasa utekelezaji wa kazi ya ukarabati imefikia asilimia 50 na baadhi ya sehemu fundi anashindwa kuendelea wanasubiri ukaguzi wa mtaalamu wa mifumo kutoka Hazina na vifaa muhimu hususan milango na madirisha ambayo yanaendelea kutengenezwa.

Mhandisi Mashambwa amesema mradi huo wa ukarabati ulipangwa kukamilika ndani ya siku 90 lakini kama vifaa na mtaalamu wa mifumo atawahi kukagua na kuidhinisha, kazi inaweza kukamilika mapema zaidi.

Katika ukaguzi huo Katibu Tawala wa Mkoa ameambatana na Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa, Kamati ya usimamizi wa miradi na Maafisa kutoka Ofisi ya Hazina Ndogo Mkoa wa Mara pamoja na mafundi wanaotekeleza miradi hiyo.  

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Katibu Tawala Mkoa aridhishwa na ukarabati wa majengo

    September 29, 2025
  • Chakula Shuleni Mkoa wa Mara ni Lazima- Kusaya

    September 02, 2025
  • Mwenge wa Uhuru Wapitisha miradi 68 ya bilioni 26.5 Mara

    August 23, 2025
  • RC Mtambi akutana na viongozi wa dini na kuwasistiza kuhamasisha amani

    August 22, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa