• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Dkt. Nyansaho Makamu Mwenyekiti Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara

Posted on: January 6th, 2026

Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ameongoza kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara kilichofanyika katika ukumbi wa uwekezaji na kumchagua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Rhimo Nyansaho kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara.

Uchaguzi huo umefanyika baada ya Mhe. Mtambi kuwasilisha jina la Dkt. Nyansaho, ambaye ni kati ya wabunge sita walioteuliwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kumpendekeza kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara na baadaye kupitishwa kwa kauli moja na wajumbe wa kikao hicho.  

“Kama wajumbe mtaridhia, mimi ninampendekeza Dkt. Rhimo Nyansaho Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara” alisema Mhe. Mtambi kabla ya wajumbe kuridhia kwa kauli moja mapendekezo hayo.

Hata hivyo, kwa kuwa Mhe. Nyansaho hakuwepo katika kikao hicho, Mhe. Mtambi alimpendekeza Mbunge wa Butiama Dkt. Wilson Charles Mahera kuwa Makamu Mwenyekiti wa kikao cha leo na wajumbe wa kikao hicho wakaridhia.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mhe. Mtambi amekumbushia agizo la kikao kilichopita kuhusu TEMESA kujenga jengo la kupumzikia abiria katika eneo la Kinesi Wilayani Rorya wakati wakisubiri usafiri katika kivuko cha MV Musoma kuja eneo la Mwigobero Manispaa ya Musoma.

Mhe. Mtambi ameiagiza TAKUKURU kufuatilia usimamizi na makusanyo wa kivuko cha MV Musoma baada ya Meneja wa TEMESA Mkoa wa Mara kukieleza kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara kuwa makusanyo ya kivuko hicho kwa mwaka ni shilingi milioni 150.  

Wakati huo huo, Mhe. Mtambi amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha kuwa TARURA inapata ofisi katika Wilaya zote za Mkoa wa Mara ili iweze kutoa huduma kwa uhakaika kwa wananchi wa Mkoa wa Mara.

Aidha, Kanali Mtambi amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kuunda timu ya wataalamu ya kufuatilia majengo ya Serikali yaliyopo katika eneo la Makao Makuu ya Wilaya ya Rorya yanayoweza kutumika kama ofisi za TARURA Wilaya ya Rorya ili kuiwezesha TARURA kuwa na ofisi katika majengo ya Serikali.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti, Wabunge wa Mkoa wa Mara walishiriki kikao hicho wamempongeza Dkt. Nyansaho kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara na kuahidi kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake hayo.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Mary Daniel akizungumza wakati akichangia hoja katika kikao hicho amempongeza Mhe. Dkt. Nyansaho kwa kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mara na kuahidi kwa niaba ya wabunge wa Mkoa wa Mara kutoa ushirikiano.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mary Daniel ameiomba TARURA kutoa fedha za matengenezo ya barabara kwa kuzingatia urefu wa barabara zinazohudumiwa katika Wilaya husika ili kutengeneza barabara hizo kwa kufuata uhalisia wa hali ya barabara zilizopo katika wilaya husika. 

Ametolea mfano wa Wilaya ya Serengeti ambayo ina zaidi ya kilimita 900 ya mtandao wa barabara kupangiwa bajeti sana na Wilaya zenye mtandao mdogo wa barabara jambo ambalo amesema linaifanya wilaya hiyo kutokuwa na barabara nzuri kwa muda mrefu.  

 Kikao hicho kimehudhuriwa na Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Mkoa, wabunge, Meya, Wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara, Maafisa kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara na Mkoa wa Kipolisi wa Tarime Rorya, TARURA, TANROADS, SENAPA, TEMESA na LATRA.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Tume ya Uchunguzi ya Matukio ya wakati na baada ya uchaguzi yaingia Mara

    January 08, 2026
  • Mara yaweka mikakati kukomesha ukeketaji

    January 06, 2026
  • Mara haitamvumilia atakayeyumbisha sekta ya elimu: Mtambi

    January 06, 2026
  • Kutupa taka ovyo Mara ni hujuma za kiuchumi: Mtambi

    January 06, 2026
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa