• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Chakula Shuleni Mkoa wa Mara ni Lazima- Kusaya

Posted on: September 2nd, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya leo ameongoza kikao cha Mkoa cha kupitia Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto tarehe 02 Septemba, 2025 kilichofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji na kusistiza msimamo wa Mkoa wa Mara kuhusu utoaji wa chakula shuleni.

Akizungumza katika kikao hicho, Ndugu Kusaya amesema kwa sasa katika Mkoa wa Mara utoaji wa chakula shuleni ni lazima kwa wanafunzi wote kupata chakula na sio jambo la kujadili tena bali Halmashauri zitekeleze.

“Utoaji wa chakula shuleni ni maelekezo ya Serikali na ni jambo ambalo linalinda haki za watoto ili kuwawezesha kupata elimu vizuri, kwa Mkoa wa Mara hatutarudi nyuma tena Mkuu wa Mkoa alishatoa maelekezo, tutekeleze” amesema Ndugu Kusaya.

Ndugu Kusaya ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Wilaya ya Serengeti kwa kufanikisha kuhamasisha wazazi na walezi katika uchangiaji wa chakula shuleni na kwa sasa watoto wote wa Halmashauri hiyo wanapata angalau mlo mmoja kwa siku.   

Aidha, Ndugu Kusaya amewakumbusha Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara kuandaa mabango yenye takwimu za utoaji wa chakula shuleni katika Halmashauri zao na kuyabandika ofisini kwao kama alivyoelekeza Mkuu wa Mkoa katika vikao vya awali.

Bwana Kusaya amewataka Wakurugenzi kuhakikisha kuwa watoto wote wanapata chakula na wazazi wote wanachangia chakula cha watoto wao wanapokuwa shule na kuwachukulia hatua wale wote ambao hawataki kuchangia chakula cha watoto.

Wakati huo huo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara amepiga marufuku wanafunzi kushiriki ngoma na nyimbo ambazo haziendani na tamaduni na maadili ya Kitanzania na hususan katika matamasha na sherehe mbalimbali.

Bwana Kusaya amesema wanafunzi wote wa shule za msingi, sekondari na vyuo wasihusishwe na ngoma na nyimbo ambazo zinawadhalilisha na badala yake jamii iwaache wakikua watacheza wenyewe wakiwa na akili timamu.  

Ndugu Kusaya amewataka Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa wa Mara kufanya vikao na wadau kuhusu Programu ya Jumuishi ya Malezi na Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto ili kupata taarifa jumuishi ya Halmashauri zao kuhusu utekelezaji wa programu hiyo.

Kwa upande wake, Afisa Lishe Mkoa wa Mara Bibi Grace Martin Mgongolwa amezipongeza Halmashauri kwa kuboresha utoaji wa chakula shuleni na kuzitaka kujikita zaidi kwenye utoaji wa chakula kwa wanafunzi wote na sio baadhi ya wanafunzi.

Bibi Mgongolwa ametoa mfano wa taarifa zilizowasilishwa kuwa kati ya wanafunzi 663,355 wa shuke za msingi za Mkoa wa Mara, wanafunzi 457,656 ambao ni sawa na asilimia 64 ndio wanapata chakula shuleni huku wanafunzi wengine hawapati chakula.

Bibi Mgongolwa amezitaka Halmashauri kuendelea kuhamasisha makundi mbalimbali ili kutekeleza afua ya uchangiaji wa chakula shuleni na kuwawezesha watoto wote kupata angalau mlo mmoja wakiwa shuleni.

Amezitaka Halmashauri kuwatumia wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao wengi wao wamejengewa uwezo katika masuala ya lishe na afya kwa ujumla ili waweze kusaidia katika kuhamasisha wananchi katika maeneo yao.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Serengeti Bwana Maulana Adam Kitambazi amesema  Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti imefanikiwa kuhamasisha wazazi na walezi katika uchangiaji wa chakula shuleni kutokana na jitihada mbalimbali zilizochukuliwa na Halmashauri.

Bwana Kitambazi amesema Halmashauri ilitoa elimu kwa viongozi wa kimila na wazee maarufu, viongozi wa dini ambao wanasauti katika jamii ambao kwa sasa wanatumika kuwahamasisha wananchi kuchangia chakula shuleni.

“Kwa sasa shule zetu kwa asilimia 100 zinatoa chakula shuleni na wanafunzi wanaonyesha utofauti hata mahudhurio na ufaulu wao umeboreka ukilinganisha na hapo awali” amesema Bwana Katambanzi.

Aidha, amesema Halmashauri ilitunga sheria ndogo zinazowabana wananchi kuchangia chakula shuleni ambazo zinasimamiwa na Maafisa Watendaji wa Vijiji na Kata katika maeneo yao ambapo amesema wananchi waliokuwa hawachangii chakula shuleni wamekuwa wakilipishwa faini.

Bwana Katambazi amesema Maafisa Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii walikuwa wanashiriki vikao vya wazazi katika shule zote ili kutoa elimu kwa wazazi hao kuhusu faida za watoto kupata chakula wakiwa shuleni.

Katika kikao hicho, Halmashauri za Mkoa wa Mara na baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo ni wadau wa utekelezaji wa programu hiyo wamewasilisha taarifa za utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Mtoto katika kipindi cha Januari hadi Juni, 2025.

Walioshiriki kikao hicho ni baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Mkoa na Maafisa Makatibu Tawala wa Wilaya, Waurugenzi wa Halmashauri, baaddhi ya maafisa wa Halmashauri, wadau mbalimbali wanaoshirikiana na Halmashauri katika utekelezaji wa programu hiyo.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Chakula Shuleni Mkoa wa Mara ni Lazima- Kusaya

    September 02, 2025
  • Mwenge wa Uhuru Wapitisha miradi 68 ya bilioni 26.5 Mara

    August 23, 2025
  • RC Mtambi akutana na viongozi wa dini na kuwasistiza kuhamasisha amani

    August 22, 2025
  • Wananchi Rorya wahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia

    August 19, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa