• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

CCM yapongeza ufaulu Sekondari ya Nyanduga

Posted on: July 26th, 2021

Kamati ya siasa ya Mkoa wa Mara imeipongeza Shule ya Sekondari ya Nyanduga kutokana na ufaulu wa wanafunzi katika matokeo ya kidato cha sita mwaka 2021.

Akizungumza wakati wa kutembelea mradi wa maabara ya somo la biolojia katika shule hiyo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Mheshimiwa Samweli Kiboye ameeleza kuwa shule hiyo imekuwa inafanya vizuri kwa muda mrefu na mara nyingi amekuwa akiwapatia zawadi kwa sababu ya ufaulu.

“Mimi kwa muda mrefu tangu nikiwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Rorya nimekuwa nikiwapa ng’ombe na kilo 200 za mchele ili kuwahamasisha wanafunzi wafanye vizuri zaidi” alisema Mheshimiwa Kiboye.

Aidha ameipongeza shule hiyo kwa matokeo mazuri waliyoyapata na kuwahamasisha wanafunzi kukazana kusoma kwani walimu wa shule hiyo wanaonekana kuwa wapo vizuri katika ufundishaji.

Wakati huo huo Mheshimiwa Kiboye ametoa ng’ombe mmoja, mchele kilo 200 na maharage kilo 40 na kuahidi kukabidhi vitu hivyo tarehe 25 Julai 2021 asubuhi ili wanafunzi wa shule hiyo waweze kusherekea matokeo mazuri ya wenzao wa kidato cha sita.

Katika kuunga mkono sherehe hiyo Mbunge wa Rorya ameahidi kutoa Kuku 20, mbuzi watatu na kukamilisha darasa moja lililoanza kujengwa katika shule hiyo.

Aidha Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Rorya ameahidi kutoa mafuta ya kupikia  na maji katoni 50 kwa ajili ya sherehe hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Salum Hapi ameahidi kutoa shilingi 1,500,000 kwa ajili ya kuunga mkono juhudi za ukamilishaji wa darasa hilo na kuahidi kuwa  Mkoa utatoa shilingi 100,000 kwa kila mwalimu wa shule hiyo aliyesababisha matokeo hayo.

Katika matokeo ya kidato cha sita Shule ya Sekondari ya Nyanduga ilipata ufaulu wa daraja la kwanza wanafunzi 20 daraja la pili wanafunzi 39 na daraja la tatu wanafunzi  watano huku kukiwa hamna daraja la nne na sifuri katika shule hiyo ambayo ni ya serikali.

Katika matokeo hayo Mkoa wa Mara ulifanya vizuri na kushika nafasi ya tatu kitaifa huku Shule ya Sekondari ya Natta ambayo ni ya serikali iliyopo katika Wilaya ya Serengeti ikishika nafasi ya kwanza kimkoa katika ufaulu na kuingia katika shule 20 bora kitaifa katika matokeo hayo.

Matangazo ya Kawaida

  • WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 MKOA WA MARA December 18, 2020
  • NAFASI ZA KAZI KWA WALIMU WA MASOMO YA SAYANSI, HISABATI, FUNDI SANIFU MAABARA NA LUGHA June 21, 2018
  • Mara yapaa Kimichezo July 20, 2019
  • JINSI YA KUPATA SALARY SLIP April 23, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Uthamini wa eneo la Nyatwali umefikia zaidi ya asilimia 50

    January 26, 2023
  • Biashara United yakabidhiwa kwa Mwekezaji

    January 13, 2023
  • Mara yapokea miradi ya zaidi ya milioni 200

    January 13, 2023
  • RC aagiza kukamatwa kwa wazazi ambao hawajapeleka watoto shule

    January 13, 2023
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: P.o.Box 299 Musoma

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa