• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Watumishi waaswa utunzaji nyaraka za miradi

Posted on: June 24th, 2021

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Lt. Josephine Paul Mwambashi amewaasa watumishi wa Umma wanaohusika katika kusimamia miradi ya umma kuhakikisha wanatunza nyaraka na vielelezo vyote vya miradi hususan inayohusu matumizi ya fedha.

Kauli hiyo imetolewa kwa nyakati tofauti leo tarehe 24 Juni 2021 wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika katika wilaya ya Rorya.

“Wataalamu hakikisheni mnatunza vizuri nyaraka zote za miradi ili hata zinapokuja kukaguliwa kusiwe na maswali mengi kuhusiana na utekelezaji wa mradi” ameeleza Mwambashi.

Amempongeza Mkuu wa Shule Sekondari ya Nyathorogo Mwalimu George Thobias Minanago kwa utunzaji mzuri wa nyaraka na vielelezo mbalimbali vinavyohusiana na ujenzi wa mradi wa vyumba viwili vya madarasa.

“Mara nyingi tunaamini wanawake ndio wasimamizi wazuri wa miradi lakini leo  mwalimu ametuonyesha kuwa hata wanaume wanaweza kusimamia miradi vizuri na kutunza nyaraka vizuri, ninakupongeza sana” alisema Mwambashi  

Aidha amepongeza pia uhifadhi wa nyaraka katika Kituo cha Afya Utegi kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya ambacho Mwenge wa Uhuru umekizindua leo.

Mwenge wa Uhuru leo umetembelea kiwanda cha viatu vya ngozi cha Credo Leather Industry; mradi wa barabara ya Tingirime hadi Nyanchabakenye;  na baadaye ukazindua kiwanda cha mafuta ya kupikia ya alizeti cha Nyihita Sunflower Cooking Oil Production kilichopo katika eneo hilo hilo la Nyanchabakenye.

Baada ya hapo mwenge uliweka jiwe la msingi katika Shule ya Sekondari  ya Kuruya na kuzindua madarasa mawili yaliyojengwa na Serikali na kukagua klabu ya kupambana na kuzuia rushwa katika Shule ya Sekondari ya Nyanthorogo .

Aidha Mwenge wa Uhuru umetembelea Shule ya Msingi Utegi kuangalia utunzaji wa mazingira na wakimbiza mwenge kitaifa walipata wasaa ya kupanda miti ya kumbukumbu katika viwanja vya shule hiyo.  

Wakati huo huo, Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru amekataa kuuzindua mradi wa maji katika shule ya Sekondari ya Buturi kutokana na mapungufu mbalimbali ikiwemo utunzaji wa nyaraka za mradi huo pamoja na utata katika uandishi wa madai ya malipo ambapo watoa huduma hawakutaja aina na kiasi cha bidhaa vilivyokuwa vinanunuliwa.  

Amemuagiza Kamanda wa Taasisi ya Kudhibiti na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza vielelezo na nyaraka za mradi huo na kutoa taarifa za awali leo jioni.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Rorya amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya pamoja na menejimenti yake kutoa maelezo kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo siku ya Jumatano tarehe 29 Juni 2021 ofisini kwake.

Mbio za Mwenge wa Uhuru katika wilaya ya Rorya zimehitimishwa jioni hii kwa mkesha wa mwenge ambao unafanyika katika mji wa Utegi na kesho unatarajiwa kukabidhiwa katika Wilaya ya Musoma.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.