• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Wananchi Mara watakiwa kuchangamkia fursa

Posted on: June 22nd, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally S. Hapi amewataka wananchi wa Mkoa wa Mara kuchangamkia fursa zinazoletwa na serikali katika mkoa huu ili waweze kujiletea maendeleo yao.  

Mheshimiwa Hapi ametoa kauli hiyo leo kwa nyakati tofauti tofauti  baada ya kuwasili mkoani Mara kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara hivi karibuni.

 “Mradi wa Chuo Kikuu ni mkubwa, na fedha zinazoletwa kwa ajili ya mradi huu ni nyingi sana na wananchi tukichamngamkia fursa zinazoletwa na mradi huu Butiama mpya inawezekana” alisema Mheshimiwa Hapi.

Ameeleza kuwa wanafunzi na watumishi wanaotarajiwa kuja ni wengi na kutokana uwingi wa watu wenye kipato Wilaya ya Butiama itakua katika uchumi wa watu wake, mapato ya halmashauri na serikali kwa ujumla.

Mheshimiwa Hapi amesema anamshukuru Mungu kwa kuhamishiwa katika Mkoa huu wa kihistoria ambapo alizaliwa na kuzikwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Nimeona kuwa Rais amenipa heshima kubwa sana kuja hapa, sehemu ambayo ni kitovu cha Baba wa Taifa, amezaliwa hapa, amekulia hapa na kuzikwa hapa, na historia kubwa aliyoiacha katika eneo hili” alisema Mheshimiwa Hapi.

Amewaahidi wazee wa Wilaya ya Butiama waliokuja kumpokea kuwa atahakikisha viongozi wa Mkoa wa Mara wanaishi fikra, maono na misingi ya Baba wa Taifa ambayo ni pamoja na uzalendo, utu, usawa na uwajibikaji katika utendaji wao.   

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mheshimiwa Anarose Nyamubi ameeleza kuwa kwa sasa ujenzi wa Chuo cha Kilimo, Sayansi na Teknolojia cha Mwalimu Nyerere unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa.

“Tayari Benki ya Dunia imeridhia kutoa  fedha  katika ujenzi wa Chuo  Kikuu cha Mwalimu Nyerere cha Kilimo, Sayansi na Teknolojia ambacho makao makuu yake yapo katika Wilaya ya Butiama” amesema Mheshimiwa Nyamubi.

Mheshimiwa Nyamubi ameeleza kuwa katika fedha zilizoidhinishwa kwa sasa hamna zilizopangwa kwa ajili ya makazi ya wanachuo na watumishi hivyo amesema kuwa wananchi wa Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla wanaweza kuwekeza katika ujenzi wa nyumba, hoteli na hosteli  za kuwachukua wanafunzi na watumishi wa Chuo hicho.  

Mheshimiwa Nyamubi ameeleza kuwa mbali na mradi huo, miradi mingine inayojengwa Butiama ni pamoja na mradi mkubwa wa Maji, mradi wa Chuo cha VETA,mradi wa hospitali mpya ya Wilaya ya Butiama na miradi mingine.

Aidha ameeleza kuwa kwa sasa Wilaya ya Butiama ina migodi ya kati miwili inayofanyakazi na  Shirika la Madini nchini (STAMICO) limeanza kuufufua uliokuwa mgodi wa Meremeta ambao ulikuwa umefungwa kwa muda mrefu na ina wachimbaji wadogo wengi wa dhahabu na madini mengine.

“Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, kwa sasa madini yanaing’arisha Butiama, na mgodi wa Meremeta ukianza utaongeza fursa zaidi kwa wananchi wa Butiama na Mkoa wa Mara kwa ujumla” alisema Mheshimiwa Nyamubi.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Mtambi ataka maboresho maandalizi ya UMISETA/UMETASHUMTA

    July 08, 2025
  • Mtambi awapongeza 2,891 kwa kupata daraja la kwanza

    July 08, 2025
  • Mita mpya kupunguza malalamiko ya bili za maji- BUWSSA

    July 04, 2025
  • Chanjo na Utambuzi wa mifugo kuwanufaisha wafugaji -Dkt. Ashatu

    July 04, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.