• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Tume ya Uchaguzi yakutana na Wadau Mara

Posted on: November 25th, 2023

Tume ya Taifa ya Uchaguzi leo tarehe 20 Novemba, 2023 imekutana na wadau wa uchaguzi katika Mkoa wa Mara kwa ajili ya maandalizi ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkutano uliofanyika katika Wilaya ya Rorya.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bwana Ramadhani Kailima amewataka wadau wote kutoa ushirikiano katika kufanikisha zoezi hili la majaribio linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 24-30 Novemba, 2023.

“Lengo la na zoezi hili ni kuvifanyia majaribio vifaa na mfumo  wa uchaguzi katika mazingira halisi ili kuweza kubaini changamoto kama zipo na kuzifanyia kazi kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025” amesema Bwana Kailima.

Bwana Kailima ameeleza kuwa zoezi la uboreshaji litahusisha kuwaandikisha wananchi wa Tanzania wenye umri wa miaka 18 na zaidi na watakaotimiza miaka 18 kabla au ifikapo tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na wapiga kura wanaoboresha taarifa zao.

Ameeleza kuwa Tume ya Uchaguzi inatarajia kutumia mfumo wa VRS katika uandikishaji wa wapiga kura na zoezi hilo litafanyika kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni na kuwa Tume imejipanga kutumia njia mbalimbali kutoa elimu kwa wananchi.

Zoezi la majaribio la uboreshaji wa Daftari la Wagiga kura litafanyika katika Kata ya Ikoma, Halmashauri ya Wilaya ya Rorya Mkoa wa Mara na Kata ya Ng’ambo, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mkoa wa Tabora.

Bwana Kailima ameeleza kuwa jumla ya vituo vya kujiandikishia 16 vimetengwa kwa ajili ya zoezi hili ambapo  vituo 10 vipo katika Kata ya Ng’ambo  (Tabora) na vituo sita vipo katika Kata ya Ikoma (Mara) na vinaweza kuongezeka au kupungua kama kutakuwa na mahitaji ya kufanya hivyo.  

Tume imekutana na wadau mbalimbali ikiwemo viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wahariri wa vyombo vya habari vya kijamii, viongozi wa vyama vya watu wenye ulemavu, waandishi wa habari, wazee maarufu na viongozi wa mila.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.