• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Tamisemi yazitaka Shule za Ufundi Kufundisha kwa Vitendo

Posted on: January 22nd, 2021

Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mheshimiwa Suleiman Jafo amezitaka shule za sekondari za ufundi zilizopo hapa nchini kutoa elimu kwa vitendo, kufanyakazi kwa weledi na ubinifu ili kuweza kuwaandaa wanafunzi wanaosoma katika shule hizo kwa ajili ya Tanzania ya Viwanda.

Mheshimiwa Jafo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Maafisa Elimu wa Mikoa, Halmashauri na Wakuu wa Shule na walimu wapya walioajiriwa katika shule tisa za sekondari za ufundi zilizopo hapa nchini leo tarehe 22 Januari 2021 kupitia mtandao wa video.

“Shule hizi kwa sasa zimeboreshwa sana kuanzia miundombinu hadi wataalamu wa kufundisha hivyo ni matarajio yetu (TAMISEMI) kuwa zitajikita zaidi kwenye kufundisha kwa vitendo ili vijana wanaofundishwa watoke wakiwa wanaujuzi wa kutosha kuweza kutumika kwenye Tanzania yaViwanda” alisema Mheshimiwa Jafo.

Mheshimiwa Jafo ameeleza kuwa wakati serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani kwa mara ya kwanza, shule hizi zilikuwa na miundombinu chakavu, hazina walimu wenye utaalamu wa ufundi na hazikuwa na vifaa vya kufundishia.

Mheshimiwa Waziri ameeleza kuwa kwa sasa shule hizi zimekarabatiwa na serikali imetumia shilingi zaidi ya shilingi bilioni 16 kukarabati shule hizi tayari serikali imeajiri wataalamu 150 wa ufundi mbalimbali kuanzia Novemba 2020 ambao tayari wapo mashuleni ili kuboresha ufundishaji katika shule hizi za ufundi.

Aidha Mheshimiwa Jafo ameahidi serikali kupeleka shilingi milioni 30 kwa kila shule ya ufundi kwa ajili ya kununua au kukarabati vifaa vya kujifunzia na kufundishia ili kuimarisha elimu inayotolewa katika shule hizo.

Aidha amezitaka halmashauri kuwalipa mara moja posho ya kijikimu walimu wote waliopangiwa katika hizi shule za ufundi ili waweze kujikimu wakati jitihada za kuingizwa katika mifumo ya mishahara zikiwa zinaendelea.

Mheshimiwa Waziri pia amewataka Wakuu wa Mikoa ambapo shule hizo zipo wawe walezi wa shule hizo na kusisimamia kwa ukaribu shule hizi ili ziweze kuleta manufaa yanayotarajiwa katika mikoa yao.

Mheshimiwa Jafo pia amewataka Wakuu wa Shule za Ufundi kuwahusisha mafundi mahiri waliopo katika mikoa yao katika ufundishaji wa wanafunzi kwa vitendo  ili wanafunzi wanaosoma katika shule hizi waweze kufaidika na umahiri wa mafundi hao.   

 Shule za sekondari za ufundi hapa nchini ni pamoja na Shule ya Ufundi Chato (Geita), Shule ya Ufundi Mwadui (Shinyanga), Shule ya Ufundi Musoma (Mara), Shule ya Ufundi Moshi (Kilimanjaro) na shule ya Ufundi Bwiru (Mwanza). Shule nyingine ni Shule ya Ufundi ya Tanga (Tanga), Shule ya ufundi Iyunga (Mbeya), shule ya Ufundi Ifunda (Iringa) na  Shule ya Ufundi Mtwara (Mtwara).  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.