• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

TAMISEMI yaitaka Mara kukamilisha Kituo cha Afya Magoma

Posted on: April 27th, 2020

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Joseph Nyamhanga ameutaka uongozi wa Mkoa wa Mara kuhakikisha unakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Magoma kabla ya Juni 30, 2020 ili kuhakikisha fedha iliyotolewa na serikali inatumika katika muda uliopangwa.  

Akizungumza leo tarehe 20 Aprili katika ziara ya kukagua maendeleo ya kituo hicho, Mhandisi Nyamhanga ameeleza kuwa tayari serikali imetoa fedha yote ya kukamilisha ujenzi wa kituo hicho na sasa kinachobakia ni utekelezaji tu wa kazi za ujenzi.

“Serikali imeshatoa zaidi ya shilingi milioni 500 tangia mwezi Desemba 2019 na mpaka sasa bado kuna kazi kubwa inahitajika kuweza kukamilisha kituo hiki” alisema Eng. Nyamhanga.

Aidha aliupongeza uongozi wa Mkoa kwa kuweza kukamilisha jengo la OPD ambalo limeanza kutumika kutoa huduma kwa wananchi wakati ujenzi wa majengo mengine ukiwa katika hatua mbalimbali.

Akijibu maombi ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kuhusu uhaba wa watumishi wa afya, Eng. Nyamhanga amesema anafahamu ikama ya Kituo cha Afya inataka kuwe na wafanyakazi 52 na kituo hicho kwa sasa kina watumishi wawili tu na kuahidi kuisaidia halmashauri kuleta wataalamu zaidi wa afya ili waweze kuletwa katika kituo hicho cha afya.  

Kwa upande wake Bwana Jackson Julius Kaimu Mtendaji wa Kijiji cha Magoma ambaye ni msimamizi mkuu wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Magoma, ameeleza kuwa mpaka sasa fedha iliyokwisha kutumika ni shilingi 220,936,243 kwa ajili ya ujenzi wa majengo hayo na zaidi ya shilingi 343,272,800 bado zipo banki.

Aidha ameeleza changamoto kubwa walioipata wakati huu wa mvua ni namna ya kuleta vifaa vya ujenzi katika eneo la ujenzi kutokana na ubovu wa barabara na mvua inayoendelea kunyesha. “Barabara ya kufika eneo hili ni mbovu sana na inatukwamisha sana katika shughuli za ujenzi” alisema Bwana Julius.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Dkt. Joseph Ngowi ameeleza kuwa awali kituo hicho hakikuwa katika bajeti ya dawa na vifaa tiba kwa mwaka huu wa fedha 2019/2020 lakini tayari Halmashauri imetenga bajeti katika mwaka wa fedha wa 2020/2021 ambayo tayari imeshapitishwa na Bunge.

“Kwa kipindi hiki cha mpito, tumefanikiwa kupata vifaa tiba, dawa na watumishi wa kuanzia kutoa huduma katika kituo hiki kutoka katika vituo vya afya na zahanati zilizopo hapa wilayani” alisema Dkt. Ngowi.

Kituo cha Afya Magoma kilipokea awamu ya kwanza ya fedha kutoka serikalini mwaka 2018 ya kujenga jengo la OPD ambapo ujenzi wake umeshakamilika na kuanza kutoa huduma aidha kimepokea awamu ya pili ya fedha Desema 2019 na ujenzi wa majengo yake upo katika hatua mbalimbali.

Katibu Mkuu TAMISEMI yupo katika ziara ya siku tatu katika Mkoa wa Mara kutembelea miradi mbalimbali na kukagua shughuli za maendeleo katika Wilaya za Tarime, Serengeti na Bunda.  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.