• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

TAKUKURU MARA YAKAGUA MIRADI 30

Posted on: November 17th, 2023

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa Wa Mara leo imetoa taarifa kwa Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara kuhusu shughuli walizozifanya katika kipindi cha Julai hadi Septemba, 2023 ambapo imekagua miradi 30 yenye thamani ya zaidi shilingi bilioni 12.4 katika sekta za afya, elimu, maji, barabara na utawala.

Taarifa iliyotolewa na Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Bwana Fidelis Kalungura na kuwasilishwa kwa waandishi wa habari na  Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mara Bwana Antony Gang’olo imeeleza kuwa jumla ya miradi mitatu kati ya miradi yote iliyokaguliwa ilikutwa na dosari.

Miradi yenye dosari ni pamoja  na mradi wa ujenzi wa miundombinu ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Buturi, Wilaya ya Rorya, ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa na matundu matatu ya vyoo katika Shule ya Msingi Kamimange Wilaya ya Butiama na Ujenzi wa Kituo cha Afya Machochwe.

Bwana Gang’olo ameeleza kuwa katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Machochwe “mradi huu umejengwa chini ya kiwango, ununuzi wa vifaa vya ujenzi haukuzingatia mahitaji ambapo baadhi ya vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 6.2 vimebakia, ambayo ni hasara kwa serikali”.

Akizungumzia mradi wa Kituo cha Afya Machochwe, Bwana Gang’olo ameeleza kuwa mradi huo una viashiria vya rushwa na uchunguzi na tayari umeanzishwa.

Aidha katika mradi wa Shule ya Msingi Mamimange Wilaya ya Butiama, vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi 4,660,000 vilivyonunuliwa viliingizwa katika vitabu lakini havikupokelewa, hali ambayo imechelewesha kukamilika kwa mradi.

Bwana Gang’olo ameeleza kuwa katika mradi wa ujenzi wa miundombinu ya Kidato cha tano na sita katika Shule ya Seondari Buturi, Wilaya ya Rorya, tofali 800 za shilingi 1,600,000 hazikuwa na ubora, TAKUKURU ilielekeza tofali hizo zisitumike katika ujenzi huo na ikawa ni hasara kwa mkandarasi.

Aidha taarifa hiyo imeonyesha kuwa TAKUKURU imefanya uelimishaji wa jamii kupitia njia ya uimarishaji wa klabu za wapinga rushwa 62 za shule za msingi, Sekondari na vyuo vya kati; mikutano ya hadhara 48, semina 45 na imeshiriki katika maonesho tisa na jumla ya watu walioelimishwa katika kipindi hicho ni 9247.

Aidha Bwana Gang’olo ameeleza kuwa jumla ya malalamiko 128 yamepokelewa katika kipindi hicho na kati ya malalamiko hayo, 76 yalihusu vitendo vya rushwa, 52 hayakuhusisha vitendo vya rushwa na malalamiko yote yameshughulikiwa.

Aidha, mashtaka mapya 3, jumla ya kesi 20 ziliendeshwa katika mahakama mbalimbali katika Mkoa wa Mara ambapo  kesi 12 zilitolewa maamuzi na upande wa Jamhuri ilishinda kesi sita na kesi sita  washtakiwa waliachiwa huru.  

Taarifa hii ni mwendelezo wa utaratibu wa kawaida wa TAKUKURU kutoa taarifa za utekelezaji wa majukumu yake katika kira baada ya miezi mitatu.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.