• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Shirikianeni na viongozi kutatua kero- Mzee

Posted on: January 30th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee leo amezungumza na viongozi wa wananchi wa eneo la Ghuba ya Speke, katika Kata ya Nyatwali, Wilaya ya Bunda na kuwataka wananchi kuwashirikisha viongozi wa Serikali changamoto zao ili waweze kusaidiana kuzitatua.

Mheshimiwa Mungiya ameeleza hayo wakati akizungumza na viongozi wa wananchi wa Kata ya Nyatwali  katika Ukumbi wa Uwekezaji uliopo ofisini kwa Mkuu wa Mkoa na kumuomba awasaidie ili wanapoondoka katika eneo la Ghuba ya Speke wapate fidia wanazostahili na na walipwe mapema ili waweze kuendelea na majukumu yao mengine.

 “Sisi viongozi tupo hapa kwa ajili yenu, tukishirikiana mambo yote yaawezekana ikiwa ni pamoja na mambo magumu ambayo tunaweza kudhani hayawezekani lakini tukiweka nguvu zetu kwa pamoja yote yanawezekana” amesema Mheshimiwa Mzee.

Aidha, Mheshimiwa Mzee amewashukuru viongozi hao kuja kuzungumza nae na kuwataka kuwasiliana nae kama kuna changamoto nyingine yoyote itakayowapata wakati wa utekelezaji wa utwaaji wa eneo la Nyatwali.

Mheshimiwa Mzee amewataka viongozi hao kuwaelimisha wananchi wa Nyatwali kuhusiana na umuhimu wa wao kushirikiana na wathamini wakati wa kufanya uthamini wa maeneo na mali zao ili waweze kulipwa fidia stahiki kwa mujibu wa sheria.

Taarifa ya viongozi hao iliyosainiwa na Diwani wa Kata ya Nyatwali Mheshimiwa Mashimo Malongo kwa niaba ya wananchi wa Nyatwali, imeeleza kuwa wananchi wa Nyatwali wameomba Serikali kutoa nyongeza ya fidia ili wananchi watakaohamishwa waweze kujikimu baada ya kuhamisha kwa hiari katika eneo hilo.

“Wananchi wa Kata ya Nyatwali hawapingani na Serikali na wala hawakatai kuhama lakini wanamashaka juu ya fidia watakayolipwa ili kupisha uendelezaji wa eneo hilo” na kuongeza kuwa kufuatia ziara ya Mawaziri wa Kisekta katika eneo hilo, wananchi wamehamasika kuchukua fomu za utambuzi na kuthaminishwa kwa ardhi na mali wanazomiliki.

Wakizungumza na Mkuu wa Mkoa, viongozi hao wameiomba Serikali kuwalipa fidia ya ardhi sawa na bei ya ardhi inayouzwa na Halmashauri ya Mji wa Bunda ambako wengi wao wataenda kununua maeneo baada ya kuhamisha kutoka katika Kata ya Nyatwali. 

Mapendekezo mengine ni pamoja na Serikali kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu ukokotoaji wa majengo; wameomba nyongeza ya malipo ya makaburi kukidhi gharama halisi za kuhamisha makaburi; nyongeza ya fidia za mazao ya chakula, mazao ya biashara na miti; fidia za mali zisizohamishika; wapewe fidia ya usumbufu (Disturbance allowance); gharama za kuanzia makazi; fidia ya kusafirisha mifugo; fidia ya vyoo; na fidia ya vyombo vya uvuvi.

Viongozi hao wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kuhakikisha utwaaji wa eneo hilo unafanyika kwa amani na utulivu wakati wote wa zoezi la uthamini, ulipaji wa fidia na uhamaji wa wananchi.

Viongozi waliokutana na Mkuu wa Mkoa wa Mara ni pamoja na Diwani wa Kata ya Nyatwali, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Kata ya Nyatwali, Wenyeviti wa Mitaa ya  Tamau, Serengeti, Nyatwali na Kariakooo na wananchi wanne waliowawakilisha wenzao kutoka katika mitaa ya Kata ya Nyatwali.

 Serikali imeamua kulitwaa eneo la Ghuba ya Speke, katika Kata ya Nyatwali, Wilaya ya Bunda kwa ajili ya uhifadhi endelevu wa ikolojia ya Hifadhi ya Taifa ya Serengati na kulinda usalama wa wananchi wa eneo hilo ambalo lipo kandokando ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Ziwa Victoria.  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • RC atoa siku 14 wanafunzi wote Sekondari ya J. K. Nyerere wapate chakula shuleni

    July 28, 2025
  • Kusaya apokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama

    July 25, 2025
  • Mtambi ataka matumizi ya GOTHOMIS kwa asilimia 100 Mara

    July 25, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.