• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Serikali yataifisha kilo 27.5 ya dhahabu

Posted on: June 16th, 2020

Serikali imetaifisha kilo 27.5 za madini ya dhahabu yenye thamani ya shilingi bilioni 3 pamoja na gari aina ya Toyota Harrier mali ya Bwana Barwesh Gandecha Mkazi wa Jiji la Mwanza yaliyokamatwa katika eneo la Sirari katika Wilaya ya Tarime, Mkoani Mara.  

Akizungumaza na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara, Mkurugenzi wa Mashtaka nchini ambaye pia ni Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali (DPP) Bwana  Biswalo E. K. Maganga  ameeleza kuwa mbali na kutaifisha mali hizo, Bwana Gandecha pia amehukumiwa  kulipa faini ya shilingi milioni 315.

“Hukumu hiyo imetolewa jana tarehe 15 Juni 2020 na Hakimu Veronica Mgendi wa mahakama ya Wilaya ya Tarime baada ya Bwana Gadencha kufikishwa mahakamani  na kukiri makosa ya utakatishaji wa fedha na umiliki wa madini kinyume cha sheria” alisema Bwana Maganga.

Ameeleza kuwa Bwana Gandecha alikamatwa katika mji wa Sirari Mei 15, 2020 akiwa na dhahabu hiyo ambayo awali alidanganya kuwa aliingiza nchini ikitokea nchi jirani ya Kenya lakini hakuwa na nyaraka za kuonyesha kuwa madini hayo yalitokea nchini Kenya.

Bwana Maganga ameeleza kuwa uchunguzi umebaini kuwa dhahabu hiyo imepatikana kupitia mtandao haramu unaofadhiliwa na Bwana Gandecha na kuwa alijaribu kutafuta nyaraka kwa njia ya udanganyifu ili kuweza kuhalalisha umiliki wa madini hayo.

“Uchunguzi pia umebaini kuwepo kwa watumishi wa serikali katika taasisi za umma ambao walikuwa wanamsaidia Bwana Gadecha kutengeneza nyaraka za kuhalalisha umiliki wa madini hayo na taratibu za kisheria zinafuatwa juu ya watumishi hao waliohusika” alisema Bwana Maganga.

Kwa mujibu wa Bwana Maganga serikali imetaifisha jumla ya kilo 425 za dhahabu katika kipindi cha miaka mitano tangu serikali ianze kutaifisha madini yanayomilikiwa kinyume cha sheria.

Akizungumza katika kikao hicho kati ya DPP na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mara, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Adam Kighoma Ali Malima ameeleza kuwa mtu huyo alikamatwa na vyombo vya dola kutokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya vyombo hivi katika Mkoa wa Mara na wananchi ambao waliamua kutoa taarifa juu ya umiliki wa madini hayo bila kufuata sheria.

“Ninawashukuru sana kwa ushirikiano huu na niwaombe wote wanaotaka kufanya biashara ya madini katika Mkoa wa Mara kufuata sheria na taratibu ili mfanye biashara yenu kihalali bila kubughudhiwa na mtu” alisema Mheshimiwa Malima.

Mheshimiwa Malima ameeleza kuwa ufanyaji wa biashara ya madini kwa njia halali utawasaidia wafanyabiashara kufanya biashara zao kwa tija na kuwapatia maendeleo endelevu ambayo yatawanufaisha watanzania wote ambayo ndio nia ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mheshimiwa John Pombe Joseph Magufuli.  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.